Programu ya Maboresho ya Jeshi la Polisi

Ni Programu ya kuboresha utendaji wa Jeshi la Polisi inayotekelezwa na serikali chini Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza inaanza 2010/2011 hadi 2014/2015 na awamu ya pili itatekelezwa kati ya mwaka 2015/2016 hadi 2019/2020.

1.0 Kuanza kwa Programu

 • Programu hii ilianza mwaka 2006 baada ya Jeshi la Polisi kupokea ripoti ya Timu iliyohusisha watalaamu wa ndani na nje ya Jeshi la Polisi iliyofanya utafiti na kutoa mapendekezo yao kwa uongozi wa Jeshi la Polisi na Wizara ya Usalama wa Raia.
 • Timu hii iliweza kukusanya maoni toka kwa viongozi wa juu wan chi wakiwemo Marais waliokuwa madaraakni na wastaafu, Rais, Mawaziri, wanachuoni, viongozi wa vyama vya siasa na dini, wananchi wa kawaida na wadau wengine.
 •  Moja ya Mapendekezo ilikuwa ni kuanzishwa kwa Programu ya Maboresho ya Jeshi la Polisi ili kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zilizokuwa zinalikabili Jeshi la Polisi.
 • Mwaka 2007 wakati IJP aliiteua Timu ya kuratibu na kusimamia Maboresho iliyohusisha wanataaluma wa ndani ya Jeshi la Polisi wenye fani mbalimbali.
 •  Programu iliidhinishwa rasmi na Baraza la Mawaziri tarehe 31.03.2012 na kuifanya itambulike rasmi kama mojawapo ya Programu za Maboresho ya Sekta ya Umma yanayoendelea hapa nchini.

1.1 Sababu za kufanya Maboresho ndani ya Jeshi la Polisi.

Mambo kadhaa yalichaguliwa na kutekelezwa kwa Programu ya Maboresho zikiwemo:-

 •  Kubadilika na kuongezeka kwa aina, mbinu na idadi ya makosa makubwa ya jinai nchini hususan mwaka 2005 na mwanzoni mwa 2006 kulikosababisha kudorora kwa hali ya usalama wa raia na mali zao kote nchini.
 •  Kudorora kwa ufanisi katika utendaji kazi wa Jeshi la Polisi kutokana na kutumia mifumo iliyopitwa na wakati wa kuzuia na kudhibiti uhalifu, uchache wa askari, ukosefu wa mafunzo ya ujuzi, uchache wa vitendea kazi na mazingira duni ya ofisi na makazi.
 • Kupungua kwa imani ya wanachi kwa Jeshi la Polisi kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu nchini na kushuka kwa nidhamu na hadhi ya Jeshi la Polisi.
 • Tamko la Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tamko na azma ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuboresha huduma kwa wananchi kwa kufanya maboresho katika Taasisi zake zinazotoa huduma kwa umma likiwemo Jeshi la Polisi.
 • Mahitaji makubwa nay a lazima kwa Jeshi la Polisi kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika huduma za kiusalama kwa jamii, kuzuia na kudhibiti uhalifu nchini.
 • Maboresho yaliyoletwa na utandawazi ambapo Jeshi la Polisi linalazimika kushirikiana na wananchi pamoja na vyombo vingine vya ulinzi na usalama nchini na duniani kwa ujumla kudhibiti vitendo vya uhalifu ambavyo havina mipaka.

Dira na Dhima Mpya ya Jeshi la Polisi

Dira (Vision)

 •  Kuwa na Jeshi la Polisi lenye Weledi, la Kisasa na linaloshirikisha jamii katika kudumisha amani, utulivu na kuongeza kasi ya maendeleo ya nchi kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Dhima (Mission)

 • Kulinda usalama wa raia na mali zao, kusimamia utekelezaji wa sheria, kuzuia na kudhibiti uhalifu, kuwakamata watuhumiwa na kudumisha amani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vithaminiwa (Core Values)

 • Ujasiri (Courage)
 • Uadilifu (integrity)
 •  Utiifu (Loyalty)
 • Uadilifu (integrity)
 • Haki (impartiality)

2.0 Mihimili Mikuu ya Maboresho ni Ipi?

Mihimili Mikuu ya Maboresho ni Usasa, Weledi na Polisi jamii

Programu ya Maboresho ya Jeshi la Polisi inajumuisha Malengo/Maeneo gani?

Programu ya Maboresho ya Jeshi la Polisi imetafsiriwa kwneye maeneo saba (70 ya Matokeo (Key Result Areas):

 • Kuimarisha mifumo ya Utendaji kazi wa Polisi
 •  Kuboresha Sheria, Kanuni na Muundo wa Kitaasisi
 • Matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
 • Kuimarisha Menejimenti ya Rasilimali Watu
 • Ujenzi wa Miundombinu na Kupata Vifaa na Zana za Kazi za kisasa
 • Kushirikisha jamii katika Kuzuia na Kudhibiti Uhalifu
 • Menejimenti na Ushirikiano wa Programu.

2.1  Nafasi ya Mwananchi wa Kawaida katika Maboresho 

Kila mwananchi bila ya kujali Itikadi, imani,tabaka, jinsia na nafasi yake katika jamii ni mshiriki wa maboresho haya kwa kukosoa, kutoa maoni, mapendekezo pamoja na kushiriki yenye mwenyewe katika kufanikisha ufikiwaji wa malengo ya Maboresho haya. 

Mafanikio ya Maboresho ni Yapi?

Mipango na mikakati mbalimbali iliyobuniwa katika kutekeleza Mikakati ya Programu ya Maboresho kwenye Maeneo Makuu Saba imeleta mafanikio katika mihimili yote mitatu – Usasa, Weledi na Polisi Jamii. Kazi mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika Idara, Vitengo, Vikosi na Mikoa ili kufikia mafanikio haya kama ifuatavyo:-

 •  Kupungua kwa uhalifu mkubwa hususani wa kutumia silaha, wizi kwenye Taasisi za fedha, mauaji ya Albino na Vikongwe.
 •  Kuongezeka kwa imani ya wananchi na wadau wengine kwa Jeshi la Polisi kunakoridhishwa na ongezeko la taarifa za uhalifu na wahalifu toka kwa wananchi na wadau pamoja na ongezeko la misaada ya hali na mali toka kwa wananchi kwa Jeshi la Polisi.
 • Kuongezeka kwa uwezo wa Jeshi la Polisi wa kupambana na wahalifu na uhalifu hususan uhalifu mkubwa ukiwemo unyanga’anyi wa kutumia silaha, mauaji ya Albino, wizi kwenye taasisi za fedha. Hali hii imechangiwa na kuboreshwa kwa mifumo ya kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu: kuimarishwa kwa upatikanaji na ubora wa vitendea kazi, kuimarika kwa ushirikiano wa Jeshi na wananchi na kuongezeka kwa ari ya utendaji miongoni mwa watendaji kuboreshwa kwa maslahi ya Askari, Wakaguzi na Maofisa.
 • Kuimarika kwa uwezo wa utoaji wa huduma bora kwa wateja hasa kwenye baadhi ya ofisi na vituo vya Polisi.
 • Kujengeka kwa utamaduni wa kukubali kukosolewa na kukosoana na kufanya maamuzi ya pamoja na wadau kuhusu mambo muhimu ya kiulinzi na usalama.
 • Kujengeka kwa hali ya kujiamini na kuheshimika kwa Askari, Wakaguzi na Maofisa machoni pa wanajamii na wadau.
 • Kuboresha ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na wadau wengine.

Wigo wa ushirikiano baina ya Jeshi la Polisi na Taasisi zingine za Kiserikali na zisizokuwa za Kiserikali na wananchi kwa ujumla umeongezeka kuanzia ngazi ya Kitaifa hadi Vituoni. Hii imejihidhihirisha kutokana na misaada ya hali na mali inayopatikana kutoka Serikali, wananchi na kwa wadau wengine.

 

3.0 Nini Muono wa Mbele wa Maboresho?

 • Kuoanisha mipango na kazi za Maboresho na utoaji wa huduma bora kwa wateja
 • Kutumia fedha kidogo kutekeleza Maboresho kwa kurandanisha Mipango ya Bajeti sambamba na Hati ya Maboresho.
 • Kuainisha na kutekeleza kazi na mikakati inayolenga kutoa Huduma Bora kwa mteja ikiwa ni pamoja na kupeleka huduma za kipolisi hadi ngazi ya Kata kupitia Mpango wa Polisi Kata/Shehia.
 • Kuainisha na kutekeleza kazi na mikakati inayolenga kutoa huduma bora kwa mteja wa ndani ili kuwawezesha kutoa huduma bora kwa wateja wa nje.
 • Kuandaa Programu amabatano pamoja na kubuni na kutekeleza mikakati itakayoongeza uwajibikaji wa askari, wakaguzi na maofisa ili waweze kutoa huduma bora kwa wateja.

Nia Yetu

  1. NIA YETU NI:KUHAKIKISHA USALAMA, HAKI, AMANI NA UTULIVU NCHINI
  2. MALENGO YETU NI:KUFANYA KAZI NA JAMII YETU PAMOJA NA WADAU WENGINE, HIVYO JESHI LA POLISI LITAHAKIKISHA YAFUATAYO:-
   • Kupunguza uhalifu na vitendo visivyokubalika na jamii
   • Kuhakikisha kuwa wahalifu wote wanakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.
   • Kuwasaidia wananchi kuwa salama na kuwafanya wajihisi kuwa wako salama kupitia mkakati wa Ulinzi Shirikishi/ Polisi Jamii (Community Policing Programme).
   • Kufanya kazi kitaalam, kuwajali wananchi na kuwaonyesha uwajibikaji katika kutoa huduma kwa waathirika wa matukio ya uhalifu.
   • Kujenga imani na kujiamini kwa wananchi.
  3. WATU WETU (WAFANYAKAZI WA POLISI):

Maafisa wakaguzi, askari wa vyeo vyote pamoja na wafanyakazi raia ambao wanaunda Jeshi letu la Polisi ni bidhaa muhimu sana kwetu, ni lazima kuzingatia kuwa na watu sahihi, wenye taaluma sahihi na wamewekwa kwenye maeneo sahihi ili kutoa huduma ya Polisi iliyobora kwa wananchi wote Tanzania. “The Police officers and civilian staff that make up the Police Force are our greatest asset and it is important that we have the right people with the right skills in the right place to deliver the best possible police service for all Tanzania citizens.”

 1. VIPAUMBELE:KUFANYA KAZI NA JAMII YETU NA WADAU WENGINE, HIVYO JESHI LA POLISI LINATEKELEZA YAFUATAYO:
  • Kufanyakazi kwa kuzingatia maadili
  • Kutenda haki kwa kila mtu, kwa kumheshimu na bila kumuonea
  • Kutoa huduma bora (kufanyakazi kwa kiwango)
  • Kuhimiza ushirikiano kama timu bora
  • Kumfanya kila mtu awajibike
  • Kutumia rasilimali zetu kikamilifu.
 2. UTAYAJUA MABORESHO YA JESHI LA POLISI KWA UNDANI ZAIDI KAMA ILIVYOFAFANULIWA HAPA CHINI:-
MAENEO YA KUBORESHWA

ENEO LINALOLENGWA KUBORESHWA
(KRA)

MIKAKATI YA KUFIKIA LENGO
(Broad Intervention)

 MIFUMO YA KUZUIA, KUPAMBANA NA UHALIFU NA UTENDAJI WA  KAZI ZA POLISI (SYSTEMS FOR IMPROVING POLICING OPERATIONS).
 •  Kuboresha Mifumo ya Kuzuia uhalifu. (Develop and Institutionalize systems for crime prevention).
 • Kuboresha Mifumo ya Kutanzua uhalifu. (Develop and Institutionalize systems for crime solving)
 • Kuboresha mifumo ya utendaji wa ndani wa jeshi la polisi  (Develop and Institutionalize systems for Internal operation).
 SHERIA, KANUNI NA MUUNDO WA KITAASISI (LEGAL, REGULATORY AND INSTITUTIONAL STRUCTURE).
 •   Kuimarisha uwezo wa taasisi zinazosimamia Jeshi la Polisi (Strengthen the capacity of police oversight and compliance institutions);
 • Kuwezesha Mapitio na Uundwaji wa Sheria na Kanuni (Facilitate review and enactment of laws and regulation);
 • Kujenga na kuboresha muundo wa jeshi (Restructure and re-organize the force).
 

ENEO LINALOLENGWA KUBORESHWA
(KRA)

 

MIKAKATI YA KUFIKIA LENGO
(Broad Intervention)

 MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO (INFORMATION AND COMMUNICATION TECHNOLOGY).
 •  Kuimarisha na kuongeza miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Strengthen and expand ICT infrastructure);
 • Kuimarisha matumizi ya TEKNOHAMA Katika utendaji wa kazi za Polisi  (Use of ICT to re – engineer delivery of police services).
 MIFUMO YA MENEJIMENTI YA RASILIMALI WATU (HUMAN RESOURCE MANAGEMENT).
 •  Kuhuishwa Kwa Muundo wa Utumishi wa Jeshi la Polisi (Strengthen HR processes and Systems);
 • Kuimarisha usimamizi na utawala wa taarifa za Rasilimali watu (Strengthen the Management of HR information);
 • Kujenga mfumo wa uongozi (Develop TPF Leadership);
 • Kupambana na maambukizi ya UKIMWI ndani ya Jeshi la Polisi (Combat HIV/AIDS in the police force);
 • Usawa wa Kijinsia (Address Gender Inequality in the force).
 

ENEO LINALOLENGWA KUBORESHWA
(KRA)

 

MIKAKATI YA KUFIKIA LENGO
(Broad Intervention)

 MIUNDOMBINU NA VIFAA KATIKA UTENDAJI WA KAZI ZA POLISI (INFRA-STRUCTURE, TOOLS AND EQUIPMENT FOR EFFECTIVE POLICING).
 •  Kuakarabati nyumba na miundombinu iliyopo na kujenga mipya  (Rehabilitate existing infrastructure and develop new ones);
 • Ununuzi wa vitendea kazi  (Acquire new and modern tools and equipment and enhance maintenance capacity).
 USHIRIKISHAJI JAMII KATIKA ULINZI NA USALAMA  (INVOLVING THE COMMUNITY IN POLICING).
 •  Kuwezesha utungwaji wa Sera ya Ushirikishwaji wa Jamii katika ulinzi na usalama  (Facilitate the development of a policy framework on involvement of the community in the policing function);
 • Kuimarisha uhamasishaji wa Polisi Jamii  (Reinforce community policing awareness campaigns);
 • Kuimarisha uwezo wa Jamii katika kuzuia na kukabiliana na uhalifu (Strengthen the capacity of the community to prevent and solve crime);
 • Kuwajengea uwezo Polisi kufanya kazi na Jamii  (Strengthen the capacity of the police to work with the community).
 

ENEO LINALOLENGWA KUBORESHWA
(KRA)

 

MIKAKATI YA KUFIKIA LENGO
(Broad Intervention)

 USIMAMIZI NA URATIBU WA PROGRAMU YA MABORESHO  (PROGRAM GOVERNANCE AND MANAGEMENT ARRANGEMENTS).
 •  Kusimamia utekelezaji wa Program ya Maboresho  (Manage the implementation of the reform program );
 • Kuweka usimamizi wa Programu ya Maboresho  (Provide Oversight to the reform program)
 • Kuratibu uhusiano wa programu hii na program zingine za maboresho  (Coordinate TPFRP with other reforms);
 • Mfumo wa tathmini na ufuatiliaji wa utekelezaji wa program ya maboresho  (Monitor and evaluate implementation of the TPFRP).

 

 

 

6.  NANI ANAHUSIKA KUBORESHA POLISI

 • Kila Afisa, Mkaguzi, Askari pamoja na watumishi raia kwa jukumu alilopewa, yeye binafsi anawajibika kutekeleza kazi hiyo kwa kuzingatia NIA YETU, MALENGO YETU NA VIPAUMBELE VYETU KATIKA MABORESHO.
 • Kila Kiongozi kwa cheo, wadhifa na majukumu yake anawajibika kusimamia utekelezaji wa MABORESHO kwa mfano.  Mkuu wa Polisi Kituo/Kitengo, Mkuu wa Polisi Wilaya, Mkoa hadi makao makuu ya polisi.

HITIMISHO

 • Inawezekana ukiwa na utashi, ubunifu na uthubutu wa dhati ukaleta mabadiliko katika Kitengo/ Kituo, Wilaya/Mkoa na Makao makuu katika eneo la majukumu uliyopewa kutekeleza kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo ya Jeshi la Polisi.
 • Unachotakiwa kufanya ni kufikiri kama mwenye mali na kuthubutu kuwajibika katika majukumu uliyopewa kutekeleza kama unavyojali mali yako binafsi.
 • Tukifikiri kama wenye mali tutaweza kufikia malengo mbalimbali tuliyojiwekea