HISTORIA YA JESHI LA POLISI – TANZANIA
1885 Wajerumani walifika Tanganyika ili kutawala, waliunda kikundi cha watu kilichofanya kazi ya Polisi.
   
1916 Vita kuu ya kwanza ikiendelea Ulaya na Afrika, kundi la Maafisa 31 (NCO) kutoka Afrika Kusini wakiwa na silaha (Rifle) walifika Tanganyika kufanya kazi za Polisi.
   
1919 Tarehe 25 August 1919 Serikali ya Kiingereza ilitangaza katika Gazeti la Serikali No.Vol.1 No.21-2583 kuwa Jeshi la Polisi Tanganyika limeanzishwa rasmi. Makao Makuu ya Jeshi hilo yalikuwa Wilayani Lushoto chini ya uongozi wa Major S.T DAVIS.
   
1921 Kundi lingine la Wakaguzi kutoka Ulaya lilifika nchini Tanganyika kuanzisha shule ya Mafunzo ya Polisi huko Morogoro.
   
1925 Kituo cha kwanza rasmi cha Polisi nchini kilifunguliwa huko Lupa Tingatinga kwenye machimbo ya dhahabu Chunya.
   
1930 Makao Makuu ya Polisi yalihamishwa kutoka Lushoto kuja Dar es Salaam.
   
1949 Motorized Company sasa Field Force Unit (F.F.U) kilianzishwa nchini kurejesha amani penye vurugu.
   
1949 Vijana mbalimbali wa Kiafrika toka shule mbalimbali za Sekondari Nchini walichaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi na kuwa Wakaguzi chini ya uangalizi (Probation Inspectors).
   
1952 Kikosi cha Mawasiliano (Signals Branch) kilianzishwa katika Polisi bila kutumia nyaya za simu.
   
1958 Askari wa Polisi wa Kikie (Women Police) walijiunga na Jeshi la Polisi chini ya uongozi wa Miss. Payee.
   
1961 Tarehe 9 Desemba, 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake. Baada ya uhuru, Jeshi la Polisi lilianza kubadili mwelekeo toka katika kutumikia Wakoloni na Walengwa wakawa ni Wananchi kwa mujibu wa sera za Serikali ya Wananchi.
   
1962

Kwa mara ya kwanza nafasi ya Kamishna wa Polisi aliyekuwa Mzungu Mr. M.S Wilson – C.P, ilichukuliwa na Mwafrika
Mr. Elangwa Shaidi – C.P.

   
1962 Maafisa 10 Waafrika waliteuliwa kuchukua nafasi za wakuu wa Polisi wa Mikoa (Regional Police Commanders).
   
1964 Tarehe 26/04/1964 Tanganyika na Zanzibar ziliungana na hivyo kuunda Tanzania. Kwa hiyo Mr. Elangwa Shaidi alipandishwa cheo nakuwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IJP).
   
  Alisaidiwa na Makamishna watatu wa Polisi ambao ni:-
 
 1  Mr Edington Kisasi  Kamishna wa Polisi Zanzibar
 2  Mr. Hamza Azizi  Kamishna wa Polisi Bara.
 3  Mr. Akena  Kamishna wa Polisi CID.
  
VIONGOZI WA JESHI LA POLISI WAKATI WA UKOLONI HADI UHURU.
1916 – 1920 Major S.T. Davis.
 1920 – 1929  E.F. Brown.
 1929 – 1933  G.H. Kiram.
 1933 – 1942  F.A.B. Nicholl
 1942 – 1949  E.B. Birthray.
 1949 – 1951  W.A. Muller.
 1951 – 1958  R.E. Fouler.
 1958 – 1962  G.S. Wilson.
 1962 – 1964  E.N. Shaidi.
 
 INSPEKTA JENERALI WA POLISI TANGU MUUNGANO HADI LEO.
 
Elangwa N.Shahidi Hamza Aziz
1964 – 1970 1970 – 1973
Elangwa N. Shaidi Hamza Azizi.
 
S.H.Pundugu Philemon Mgaya
7/8/1973 – Aug 1975 8/8/1975 – Nov 1980
Samweli H. Pundugu. Philemon N. Mgaya.
 
Solomon Liani
2/11/1980 – 30/11/1984 1/12/1984 – 3/5/1996
Solomoni Liani. Harun G. Mahundi.
 
4/5/1996 – 2/3/2006 3/3/2006 - 30/12/2013
Omar I. Mahita. Saidi A. Mwema.
 
IJP Ernest Jumbe Mangu  
01/01/2014-29/05/2017 29/05/2017-Hadi Sasa 
Ernest J. Mangu Simon Nyakoro Siro 
WAKURUGENZI WA IDARA YA UPELELEZI (CID) TANGU 1960 HADI LEO.
17/9/1960-1/9/1961 M. J. McKinlay ACP.
1/9/1961-19/7/1962 K.F.J. Flood SSP.
19/7/1962-6/12/1962 R. T. L. Egan ACP.
6/12/1962-2/8/1967 E. E. Akena ACP.
2/81967-13/11/1967 R.S. Kaswende ACP.
13/11/1967-4/6/1968 N.G.M. Sawaya SACP.
4/6/1968-2/9/1968 A.R.Shungu SACP.
2/9/1968-23/9/1970 N.G.M. Sawaya SACP.
23/9/1970-21/5/1973 S.H.Pundugu CP.
21/5/1973-28/5/1975 B.M. Omari CP.
28/5/1975-14/8/1975 F.M. Mtono SACP.
14/8/1975-15/2/1977 H.M.Lyimo CP.
12/2/1977-21/5/1981 M.Mwingira CP.
21/5/1981-6/3/1985 J.M.Lemomo CP.
7/3/1985-30/6/1992 A.A.B.Mwaitenda CP.
22/10/1992-3/5/1996 E.A.Man CP.
4/5/1996-2/3/2006 Adadi Rajab CP.
3/3/2006-14/07/2013 R.S. Manumba CP.

15/07/2013 - 2014

2014-2017

I.N. Mngulu - CP

Diwan  Athuman

CP

06/02/2017- Hadi Sasa

Robert Boaz Mikomangwa

CP