• Mwombaji awe na umri wa miaka 21 na kuendelea
 • Awe na leseni halali ambayo inamruhusu kuendesha daraja analotaka kufundisha na pamoja na hati ya ushindi (certificate of competence.)
 • Mwombaji anatakiwa kwenda Ofisi ya Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa husika, au aende moja kwa moja Ofisi ya Kamanda Polisi, Usalama Barabarani (T). Na kutakiwa kujaza form ya kuomba kujaribiwa/kutahiniwa.
 • Atatahiniwa na Mkaguzi wa magari/mtahini wa madereva. Mtihani huo unalenga maeneo makuu yafuatayo:-
 1. Kupima uwezo wa kuendesha na kulimudu gari awapo barabarani.
 2. Uelewa wa Sheria ya Usalama Barabarani na kanuni za njia (highway code) pamoja na matumizi ya alama za barabarani.
 3. Uwezo wa kutoa maelekezo kwa wanafunzi wakati wa mafunzo kwa vitendo.
 4. Mwombaji atakayefaulu atapewa cheti cha ushindi iwapo atashinda.
 5. Mtahini atajaza fomu kuthibitisha uwezo wa mwombaji.
 6. Mtahiniwa atajaza fomu kwa ajili ya kuomba kusajiliwa.
 7. Usajili utatolewa na Ofisi ya Kamanda wa Polisi, Usalama Barabarani (T).

Makosa ambayo mwalimu wa madereva anaweza kunyang’anywa leseni.

 • Iwapo atakuwa ameonywa na kurudia makosa yaleyale aliyoonywa
 • Iwapo atakuwa ameadhibiwa mara mbili au zaidi kwa kosa lilelile.
 • Iwapo atapoteza sifa ya kumiliki leseni ya Udereva.
 • Iwapo atafutiwa leseni na Mahakama.

Ikumbukwe kwamba leseni hii itakuwa halali hadi hapo itakapositishwa na Jeshi la Polisi, au iwapo atakiuka Sheria ya Usalama Barabarani.