UTARATIBU WA UVUKAJI BARABARA KWA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI ZILIZOPO KANDOKANDO MWA BARABARA (JUNIOR PATROL)

Traffic Junior Patrol

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (T) SACP. MOHAMED R. MPINGA akizindua rasmi utaratibu wa uvukaji Barabara kwa wanafunzi wa shule za msingi (Junior Patrol)

 

Kutokana na ongezeko la ajali za barabarani zinazotokea mara kwa mara hasa kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizopo kandokando mwa barabara, Jeshi la polisi, kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani (T) , limebuni utaratibu wa wanafunzi kuvushana wao kwa wao kwa kutumia vibao maalum.

Mfumo huu umefanikiwa kwa kiasi kikubwa nchini Malawi na unajulikana kwa jina la ‘SCHOLAR PATROL’, na umepunguza ajali za wanafunzi kwa kiasi kikubwa,hivyo kikosi cha usalama barabarani kimeona mfumo huo ni mzuri kuigwa hapa nchini.

Baada ya wanafunzi wa baadhi za shule za Dar Es Salaam kupata mafunzo ya zoezi hili, mfumo huu ulizinduliwa rasmi na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (T) SACP. MOHAMED R. MPINGA, tarehe 29.01.2011 katika Barabara ya Ally Hassan Mwinyi. Hivyo basi zoezi hilo limeshaanza kwa shule 12 za Mkoani Dar Es Salaam na Shule 2 za mkoani Mbeya. Lengo ni zoezi hili lisambae shule zote zilizokuwa kandokando mwa barabara katika Mikoa yote Tanzania Bara.

LENGO.

  • Kupunguza ajali kwa wanafunzi ambao ndio taifa la kesho.
  • Kutekeleza mpango wa Polisi Jamii kwa kushirikisha wanafunzi kwani Mpango huu utawajengea watoto tabia ya kutii /kutekeleza sheria hususani sheria ya Usalama Barabarani, kwa kuwaandaa watoto hao kuwa madereva wazuri wa Taifa la kesho.

VIFAA VINAVYOTUMIKA KWENYE MPANGO HUO.
1. Kibao kinachotumika kuwavushia wanafunzi, Upande mmoja wa kibao chenye neno SIMAMA(STOP) na upande mwengine NENDA(GO).

nenda

 

Simama

2. Jaketi  la kuakisi mwanga  (Reflective jacket) ambalo huvaliwa na   mwanafunzi anayewavusha wenzake.

Jaketi

Jacketi la kuakisi mwanga linavyoonekana kwa nyuma linalovaliwa na mwanafunzi anayewavusha wenzake.

UTARATIBU WA UVUSHAJI WANAFUNZI ((JUNIOR PATROL)

Baada ya wanafunzi  kupata mafunzo ya utaratibu huu wa Junior Patrol kutoka Jeshi la Polisi.

JUNIOR PATROL

Wanafunzi wa shule ya Msingi Mbuyuni na kumbukumbu za Jijini Dar Es Es Salaam wakipata maelekezo ya utaratibu wa Junior Patrol toka Jeshi la Polisi.

  • Wanafunzi maalum wawili waliochaguliwa wenye zamu kwa siku ya kuwavusha wenzao kwa siku hiyo, mmoja atasimama upande mmoja wa barabara  akiwa na kibao kwa ajili ya kuvushia wenzao kwa kusimamisha magari yanayotoka kulia kwake na mwingine atasimama upande mwingine wa barabara vivyo hivyo kwa ajili ya kusimamisha magari yanayotoka kulia kwake

junior patrol

 

junior patrol

  • Wanafunzi hao watatakiwa kusimama usawa wa mstari ambao magari husimama kabla ya kufika kwenye zebra. 

Katika maeneo ambayo hakuna zebra wanafunzi hao watatakiwa wasimame sehemu ambayo ni salama kwa ajili ya kuwavushia wenzao .
 1. Wanafunzi hao watasimama kandokando mwa barabara, na kunyoosha kibao hicho kwa kutumia mikono yake miwili usawa wa barabara upande wa simama (Stop) kuashiria magari kusimama.
2 .Baada ya kuhakikisha magari yamesimama na ni salama wanafunzi wataruhusiwa kuvuka.

junior patrol

junior patrol

3. Baada ya kuhakikisha kuwa wote wamevuka salama watayaruhusu magari yapite kwa kugeuza kibao upande ulioandikwa NENDA (GO) na kuyaashiria kwa mkono wa kulia yaendelee na safari.
4. Baada ya kumaliza kuwavusha wanafunzi wenzao, wanafunzi hao kila mmoja atarejesha kibao bega la kulia.
5. Zoezi hilo la kuwavusha wanafunzi ni endelevu kila siku pale ambapo wanafunzi wanataka kuvuka.