Balozi wa Japan nchini, akikata utepe kuzindua gari maalumu la matangazo kwa ajili ya  uelimishaji alilokabidhi kwa kikosi cha usalama barabarani,(kushoto) ni Mkuu wa Kikosi cha usalama Barabarani DCP Mohamed Mpinga.

Zifuatazo ni Sheria na Kanuni za Usalama Barabarani:-

 1. GN 24-2015
 2. The Road Traffic Act

Baadhi ya viongozi wakipata mafunzo ya alama za Barabarani kwenye barabara iliyotengenezwa

 • Mwombaji awe na umri wa miaka 21 na kuendelea
 • Awe na leseni halali ambayo inamruhusu kuendesha daraja analotaka kufundisha na pamoja na hati ya ushindi (certificate of competence.)
 • Mwombaji anatakiwa kwenda Ofisi ya Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa husika, au aende moja kwa moja Ofisi ya Kamanda Polisi, Usalama Barabarani (T). Na kutakiwa kujaza form ya kuomba kujaribiwa/kutahiniwa.
 • Atatahiniwa na Mkaguzi wa magari/mtahini wa madereva. Mtihani huo unalenga maeneo makuu yafuatayo:-

 • Mwombaji anatakiwa kuwa na leseni ya Udereva ya daraja lolote lile iliyo hai ya hapa Nchini.
 • Anatakiwa kuipeleka leseni yake ofisi ya Mamlaka ya Leseni (T) TRA kwa ajili ya ukaguzi,
 • Baada ya Ukaguzi, Mamlaka ya Leseni (T) TRA itatoa barua rasmi kwenda kwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani(T) kuthibitisha uhalali wa leseni hiyo.
 • Ofisi ya Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (T) itakagua leseni hiyo pamoja na cheti cha Umahiri (Certificate of Competence) kuthibitisha uhalali wa leseni na cheti hicho cha umahiri.
 • Baada ya kuthibitisha uhalali wa leseni hiyo, Ofisi ya Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (T) itatoa barua rasmi kwenda Oisi ya Automobile Association Tanzania ambayo ndiyo asasi pekee hapa nchini yenye Mamlaka ya kutoa leseni za Kimataifa.

1.0 LESENI YA KUENDESHA GARI CHINI YA MFUMO MPYA WA LESENI

Lengo la kuanzisha mfumo mpya ni kuchukua nafasi ya mfumo wa zamani ambao hakuweza kutofautisha kati ya aina ya leseni kwa ajili ya kuendesha gari na magari ya abiria ya uwezo tofauti. Chini ya mfumo mpya daraja maalum ya leseni ya kuendesha gari imeundwa kulingana na daraja la aina ya magari tu. Wamiliki wa leseni ya kuendesha gari ya daraja fulani atalazimika kuendesha gari kulingana na  daraja  ambalo alikuwa kafanyiwa majaribio na si vinginevyo. Ili kupata leseni ya kuendesha gari mpya, watu wote lazima wapewe mafunzo katika shule ya udereva (taasisi) inayotambuliwa kabla hawajapata hizo leseni mpya. Mfumo umegawanywa katika makundi mbalimbali kulingana na uwezo wa gari yaani:

UTARATIBU WA UVUKAJI BARABARA KWA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI ZILIZOPO KANDOKANDO MWA BARABARA (JUNIOR PATROL)

Traffic Junior Patrol

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (T) SACP. MOHAMED R. MPINGA akizindua rasmi utaratibu wa uvukaji Barabara kwa wanafunzi wa shule za msingi (Junior Patrol)

Shule za udereva zinasimamiwa na sheria inayoitwa “THE DRIVING SCHOOL ACT CHAPTER 163 OF LAW OF 1965 R.E 2002”.
Sheria hii inaelezea wazi kwamba Mkuu wa Jeshi la Polisi (I.J.P) ndiye mwenye mamlaka ya kusajili shule zote za udereva Tanzania. Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani amekasimiwa madaraka hayo na I.J.P, hii ni pamoja na kubuni mikakati ya uboreshaji wa shule hizo za udereva ili kukidhi utoaji wa taaluma bora.