HISTORIA FUPI YA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA TANZANIA

UTANGULIZI:

Kikosi cha Kutuliza Ghasia Tanzania kilianzishwa mwaka 1949 na Serikali ya Uingereza mkoani Dar es saalam. Kikosi kilikuwa maeneo ya barabara ya Kilwa. Kilijulikana kama Motorised Company. Mwaka  1954 kikosi kilihamishwa kutoka barabara ya Kilwa na kupelekwa Ukonga Dar es salaam. Baadaye katika mwaka huo huo vikosi nane zaidi vilianzishwa katika mikoa nane. Mikoa  hiyo ni; Morogoro, Tanga, Mbeya, Iringa, Tabora, Kilimanjaro, Mwanza na Musoma.

 KUSUDI LA KUANZISHA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA:

 A: KABLA YA UHURU (WAKATI WA UTAWALA WA KIKOLONI)

Lengo kuu la kuanzisha Kikosi cha Kutuliza Ghasia katika Jeshi la Tanganyika (siku hizi Tanzania) ilikuwa ni kulinda maslahi ya wakoloni (British). Waingereza walikuwa na mashamba makubwa ya katani, kahawa, tumbaku na chai. Waliendesha pia shughuli za uchimbaji madini katika maeneo mbalimbali. Hivyo, walianzisha kikosi hiki ili kuleta hofu kwa wafanyakazi ambao waliokuwa wakidai mazingira/maslahi mazuri ya kazi na waliotumia migomo. Kamanda wa kikosi wakati wa ukoloni wa Uingereza alijulikana kama MR.KING:

 B: BAADA YA UHURU

Tanganyika ilipata uhuru wake mwaka 1961. Malengo ya kikosi hiki na Jeshi la Polisi Tanzania yalibadilika kutoka  kulinda maslahi ya wakoloni hadi kulinda maslahi ya Watanzania. Majukumu makubwa ya kikosi na Jeshi kwa ujumla yakawa (hadi sasa) ni kulinda raia wake / watu na mali zao.

 Mnamo mwaka 1964 ASP GEORGE BONDO (Mtanzania wa kwanza) aliteuliwa kuwa kamanda wa kikosi hiki hadi mwaka 1967. Hadi sasa tuna vikosi 31 ambavyo viko nchini kote.

Chati chini inaonyesha viongozi ambao walishawahi kuongoza kikosi kuanzia mwaka 1964 hadi sasa.

S / N

Jina

Cheo

Mwaka

1

 GEORGE BONDO  

ASP

1964 - 1967 

2

ASUMWISYE MWAKIBINGA 

SP

1967 - 1975

3

 PRASHANT ACHUTAN  

SACP

1975 - 1988

4

 SALUM G. SHABAN 

ACP

1988 - 1990

5

  BAKARI. R. KUBIHA  

SACP

1990 - 1995

6

SALUM G. SHABAN

SACP

1995 - 2006

7

JAMES A. KOMBE

SACP

2006 - 2007

8

TRESPHORY ANACLET  

SACP

2007 - 2012

9

10

FERDINAND E. MTUI 

ONESMO LYANGA

ACP

ACP

2012

SASA

 

  KAZI ZINAZOFANYWA NA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA

Kikosi cha Kutuliza Ghasia Tanzania hufanya kazi mbalimbali. Kazi hizo ni doria za mipaka, udhibiti wa mikusanyiko na usimamizi wa machafuko ya kisiasa, ulinzi wa watu mashuhuri na ulinzi wa maeneo maalum, uendeshaji na usimamizi wa Maafa, kwa kutaja machache.

  MAKAO MAKUU YA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA

Hii ndio makao makuu ya vikosi vyote vya kutuliza ghasia nchini ambavyo viko chini ya maelekezo ya jumla na amri ya mkuu wa kikosi (CO) anayehusika na kutoa usimamizi wa jumla na utawala wa vikosi vyote. Mbali na usimamizi na utawala wa makao makuu ya Kikosi kulingana na Police General Order ina jukumu la kuandaa mipango ya mafunzo na hasa kusisitiza juu ya mahitaji ya kikosi cha kutuliza ghasia. Pia katika makao makuu ya kikosi tuna  Crisis Response Team (CRT) ambayo ilianzishwa Agosti 2006, ni timu maalum ambayo inahusika na kupambana na ugaidi na makosa makubwa ya jinai nchini kote.