Mkuu wa Jeshi la Polisi, IJP Ernest Mangu akimsikiliza  Waziri wa Mawailiano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa wakati wakimsubiri mgeni rasmi kuzindua namba ya mawasiliano ya dharura ya Polisi .

 

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi, IJP Ernest Mangu akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa TCRA Bw.Joseph Kilongola wakati wa uzinduzi wa namba ya mawasiliano dharura ya Polisi.

Wananchi wametakiwa kutumia namba za Mawasiliano ya  dharura  ya Polisi 111 na 112 kutoa taarifa za vitendo vya uhalifu na wahalifu.

Jeshi la Polisi  nchini kwa kushirikiana na Mamalaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA)  limezindua  namba ya mawasilianao ya dharura  111 na 112,   kwa lengo la  kuboresha  mawasiliano  kati Jeshi la Polisi na wananchi ili kutatua kero za  uhalifu na  wahalifu.

  • Namba hizo za  Mawasiliano ya dharura kuanzia sasa zitatumika na wananchi  bila  gharama yoyote kwa kupiga au kutuma ujumbe mfupi kwa ajili ya kuripoti au kutoa taarifa zifuatazo:-
  1. Taarifa za Uhalifu na wahalifu
  2. kuripoti  matukio ya ajali
  3. Taarifa za majanga 
  •  Namba hizi zinatumika kwa Simu ya aina yoyote  kwa kupiga au kutuma ujumbe mfupi.

Wananchi wasitumia namba hizo kwa kutoa taarifa za uongo badala yake watumie namba hizi katika  kutanzua uhalifu kabla haujatendeka ili kuweza kuimarisha usalama wa raia na mali zao.