Ukiona uhalifu unatendeka toa taarifa mapema katika kituo cha Polisi  au polisi aliye karibu nawe.

  • Endapo utamtilia shaka mtu au watu usiowajua toa taarifa mapema katika vituo vya Polisi, polisi wasaidizi(auxiliary police),walinzi wa amani au ofisi ya serikali ya mtaa/kijiji.
  • Usalama wa vyombo vya usafiri kwenye maegesho, kumbuka kufunga pikipiki au baiskeri kwa mnyororo, kuweka alamu katika magari,kuondoa vitu vya thamani ndani ya gari.
  • Kuwa na zizi imara la mifugo ili kuzuia wezi na kuiweka mifugo alama
  •  Kuepuka kusafiri na kiwango kikubwa cha fedha na vitu vyenye thamani
  • Kujenga tabia ya kuweka alama kwenye vitu
  • Kutoacha vitu vya thamani katika sehemu za wazi. Hata kama ni ndani ya nyumba vitu vya thamani vifungiwe ndani ya kabati au stoo.

HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI

  •  Kusimamia sheria na kanuni za usalama barabarani mfano kudhibiti mwendo kasi, n.k
  • Kuthibitisha wanaostahili kupewa leseni za udereva
  • Ukaguzi wa magari na madereva
  • Kuongoza magari barabarani yaende kwa mtiririko unaostahili