Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amefanya mabadiliko ya Kamanda  wa Polisi  mkoa wa Kinondoni pamoja na Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga.

katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa kinondoni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Suzan Salome Kaganda amekuwa mkuu wa kitengo cha mafao  na fidia makao makuu ya Polisi,

na nafasi hiyo inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Murilo Jumanne Muliro ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga.

Aidha, nafasi ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga imejazwa na Kamishina msaidizi wa Polisi (ACP) Simon Haule ambaye alikuwa afisa mnadhimu wa Polisi mkoa wa Mara.

Uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Polisi katika kuongeza ufanisi wa  utendaji Kazi.