Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, akiwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, akitokea Nairobi nchini Kenya kuhudhuria hafla ya ufungaji wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na matishio ya kigaidi na uhalifu unaovuka mipaka kwa  Majeshi ya Polisi ambao ni wanachama wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki

(EAPCCO), kushoto ni kamishna wa Polisi Jamii Mussa Ali Mussa.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, amefanya ziara ya kikazi ya siku mbili  Nairobi nchini Kenya, ambapo pamoja na mambo mengine alifunga wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na matishio ya kigaidi na uhalifu mwingine unaovuka mipaka kwa Majeshi ya Polisi ambao ni wanachama wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO).
Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa takribani siku kumi na tatu (13) kuanzia Julai mosi hadi Julai 13 mwaka huu, yatasaidia kuongeza hali na morali kwa askari Polisi huku ikitajwa kuwa ndiyo njia pekee ya kuweza kukabiliana na matishio mbalimbali ya kiuhalifu na wahalifu.
Aidha, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, amerejea nchini na kupokelewa na Kamishna wa Polisi Jamii  (CP) Mussa Ali Mussa pamoja na Kaimu kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi ya Dar es salaam, Naibu kamishna wa Polisi (DCP) Lucas Mkondya.
Katika salamu zake kwa Jeshi la Polisi, IGP Sirro alisema kuwa, licha ya kwamba jeshi la polisi nchini ni mwanachama wa Shirikisho hilo, limejipanga kuhakikisha kuwa awamu ijayo linapeleka washiriki wa kutosha ili waweze kunufaika na mafunzo hayo yatakayo lisaidia taifa kukabiliana na matishio mbalimbali ya uhalifu na wahalifu.