Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,  IGP Simon Sirro, akizungumza na Askari wa kikosi cha kutumia ghasi (FFU) kusini  Pemba, Mara baada ya kupokea salamu ya heshima ya kijeshi. 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amefanya ziara ya kikazi katika mkoa wa kusini Pemba, huku akiwataka askari kufanyakazi katika misingi ya ueledi na uzalendo na kuhakikisha kuwa vitendo vya uhalifu na wahalifu vinakomeshwa.


Hayo ameyasema leo alipowasili mkoani hapa na kufanya kikao kazi na watendaji wa Jeshi la Polisi kutoka mkoa kaskazini na kusini Pemba huku lengo la ziara yake ukiwa ni kujitambulisha toka aliposhika nafasi ya kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini na kuchukua nafasi ya mtingulizi wake ambaye ni Mkuu wa Jeshi mstaafu Ernest Mangu.


    IGP Sirro amesema kuwa, katika hatua za kukabiliana na matukio ya kihalifu ikiwamo biashara haramu ya kusambaza na kuuza dawa za kulevya ni vyema Askari kote nchini  wakatimiza wajibu wao kwa kufuata misingi ya sheria na taratibu.


    Mapema Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi alifika ofisin ya Mkuu wa mkoa wa kusini Pemba  na kujitambulisha Mbele ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama kisiwani Pemba na kuwahakikishia kamati hiyo kuwa, Jeshi la Polisi nchini litahakikisha linaendelea kudumisha hali ya ulinzi na usalama hususan usalama wa raia na mali zao.