Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akionyeshwa moja ya gari na mkuu wa mipango wa kampuni ya Kifau, Mario Gasparri alipokabidhiwa magari manne ya msaada kutoka kampuni ya Haval Motors, Dar es salaam.

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini , IGP Simon Sirro amepokea msaada wa magari Manne kila mmoja likiwa na thamani ya shilingi 126.2 milioni kutoka kampuni ya Haval Great Wall Motors yatakayosaidia kupambana na uhalifu nchini.

wakati akipokea Magari hayo, IGP Sirro aliwahakikishia wanachi kuwa Jeshi la Polisi linaendelea vizuri na suala la mauaji ya kibiti  muda si mrefu kutakuwa na majibu mazuri.

IGP sirro alisisitiza kwamba suala la ulinzi na usalama ni la watu wote na kwamba wananchi wa maeneo ya kibiti, mkuranga na rufiji wanapaswa kujilinda kwa kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi vitakavyowezesha kuimarisha usalama wao na utoaji wa taarifa sahihi zitakazowezesha kukamatwa kwa wahalifu.