Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki (katikati) akiwaongoza maofisa, wakaguzi na askari kuimba wimbo wa maadili ya ofisa wa Polisi wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya upelelezi yaliyofanyika katika chuo cha maafisa wa Polisi kidatu mkoa wa morogoro.

 

Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki akipokewa na Kamishina wa operesheni na mafunzo, Nsato Marijani katika chuo cha maafisa wa Polisi kidatu alipokwenda kufunga mafunzo ya upelelezi kwa askari polisi wa mkoa wa kinondoni ambako mpango wa kuboresha usalama wa jamii unaendelea kutekelezwa.

Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya upelelezi Polisi Konstebo Jonathan Tossi , mafunzo hayo yalifanyika katika chuo cha maafisa wa Polisi kidatu mkoa wa Morogoro.