Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhe.Charles Kitwanga akimkabidhi Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu ripoti ya kuboresha usalama wa raia na mali zao kutoka kwa Mtendaji mkuu wa Ofisi ya raisi inayoshughulikia miradi ya BRN, Omar Issa, tukio  hilo limefanyika  Makao makuu ya Jeshi la Polisi, Dar es salaam.

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akikabibhiwa  ripoti kutoka kwa Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mhe. Charles Kitwanga kwa ajili ya utekelezaji wake.

Mtendaji Mkuu wa PDB, Omar Issa akifafanua jambo kuhusu ripoti ya kumarisha usalama wa raia na mali zao.

Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Charles Kitwanga akiagana na Mtendaji mkuu wa PDB Omar Issa, Pembeni ni Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu.