fng1

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro wakiingia ukumbini wakati wa Sherehe za Kuwapongeza na kuwaaga Wastaafu wa Vyeo mbalimbali wa Jeshi la Polisi na kuukaribisha Mwaka Mpya 2019 ( kulia) ni Kamishna wa Ushirikishwaji wa Jamii, CP Mussa Alli Mussa. Sherehe hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

fng2

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akimkabidhi zawadi Naibu Kamishna Mstaafu wa Polisi Hussein Laizer (kulia) ,Wakati wa Sherehe za kuwapongeza na kuwaaga Wastaafu wa vyeo mbalimbali wa Jeshi la Polisi na kuukaribisha mwaka mpya 2019,Sherehe hiyo imefanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

fng3

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo akiongea na Maafisa, Askari waliopo kazini na Wastaafu wa Jeshi la Polisi (hawapo pichani) kushoto ni Inspekta Jenerali wa Polisi , Simon Sirro wakati wa Sherehe za Kuwapongeza na Kuwaaga Wastaafu wa Vyeo mbalimbali wa Jeshi la Polisi na kuukaribisha Mwaka Mpya 2019, Sherehe hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

fng4

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt.Anna Makakala akiongea na Maafisa ,askari waliopo kazini na wastaafu wa Jeshi la Polisi (hawapo pichani), Kushoto ni Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro wakati wa Sherehe za Kuwapongeza na Kuwaaga Wastaafu wa Vyeo mbalimbali wa Jeshi la Polisi na kuukalibisha mwaka mpya 2019,Sherehe hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

 

 

SIRRO AWAPONGEZA WASTAAFU KUMALIZA  BILA KASHFA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro amewapongeza Wastaafu wa Jeshi hilo kwa kumaliza utumishi wa umma wakiwa hawana kashfa yoyote ambayo ingelichafua jeshi hilo na kufanya lipoteze uhalali mbele ya wananchi. IGP Sirro ameyasema hayo wakati wa Sherehe ya Kuwaaga Askari na Wastaafu wa Jeshi na Sherehe ya Kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2019 iliyofanyika katika  Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam

“Nawapongeza kwa kumaliza salama naomba mkawe na nidhamu ya fedha mtakayolipwa kama kiinua mgongo na mtumie kiasi hicho cha pesa kwa manufaa ya familia na jamii inayowazunguka” alisema IGP Sirro
 
Akizungumza katika Sherehe hizo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,  Jenerali Venance Mabeyo   amewataka Wastaafu wa Jeshi la Polisi kuhakikisha wanakuwa raia wema  na kudumisha amani katika maisha yao mapya baada ya kulitumikia Taifa kwa manufaa,ameongeza kuwa Upendo waliouonesha kwa wafanyakazi wenzao wakati wakiwa kazini wakauonyehe huko wanakoenda

“Mmekua mfano wa kuigwa kipindi chote mlichokua kazini, tunaomba mkawe raia wema huko kwa kuendelea kusimamia matukio ya uhalifu katika maeneo mtakayokua mnaishi, tunaamini nyie bado askari na mnafahamu mbinu zote za kupambana na uhalifu hivyo fahamuni tunawategemea bado,” alisema Jenerali Mabeyo
 
Maafisa na Askari Wastaafu wa Jeshi la Polisi walioagwa katika sherehe hizo walilishukuru Jeshi la Polisi kwa upendo walioupata katika kipindi cha utumishi kwa umma na kuwaasa maafisa na askari walipo kazini kulitumikia jeshi kwa uaminifu mkubwa.