Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa polisi kutoka nchi mbalimbali wanaosoma chuo cha ulinzi wa taifa cha Rwanda.

Ujumbe huo unaohusisha maofisa wa Polisi kutoka nchi za Afarika mashariki na Afrika magharibi unaongozwa na Kamishina wa Polisi wa Rwanda Felix Namhoranye ambaye ndiye mkuu wa chuo cha ulinzi cha ulinzi cha Rwanda wapo nchini Tanzania kwa ziara ya kijifunza namna taasisi mbalimbali zinavyoendeshwa hapa Tanzania. ujumbe huo utatembelea maeneo yafuatao, Bandari ya Dar es salaam, kiwanda cha kutengeza juisi cha Bakhresa, Chuo cha Diplomasia,Makumbusho ya taifa na mwisho wataenda Morogoro - mikumi.