Main Menu
Useful Links
| Tahadhari za Usalama |
| Polisi Jamii |
| Vifungu vya Sheria |
| SMS & CALLS |
Who's Online
We have 1 guest onlineLogin Form
| WATAALAM NA WAKUU WA KUZUA DAWA ZA KULEVYA NCHI ZA MAZIWA MAKUU NA PEMBE YA AFRI KUKUTANA DARA |
|
Msemaji Msaidizi wa Jeshi la Polisi nchini ASP Advera Senso, amesema kuwa, mkutano huo wa siku mbili utafunguliwa na Mkurugenzi wa Operesheni wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Paul Chagonja Jumatatu ijayo Aprili 12, 2010. Amesema mkutano huo ambao utafanyikwe kwenye Hoteli ya Regency Park Mikocheni Jijini Dar es Salaam, utafunguliwa Saa 2.15 asubuhi. Amesema kuwa pamoja na wajumbe wan chi za Maziwa Makuu na pembe ya Afrika, mkutano huo utahudhuriwa na wataalamu kutoka nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC, nchi za Jumuiya za Falme za Kiarabu UAE na Pakistan. Amezitaja nchi na mashirika ya Kimataifa yatakayohudhuria katika mkutano huo kuwa ni Nigeria, Ghana, na Makao Makuu ya Shirikisho la Polisi wa Kimataifa INTERPOL kutoka nchini Lyon Ufaransa na Nairobi inayohudumia nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika. Nchi za maziwa makuu zitakazoshiriki katika mkutano huo ni Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya, Shelisheli, Sudani, Djiout, Eritrea, na wenyeji Tanzania. Huo ni mkutano wa kwanza wa wataalam kufanyika kwa nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika na unafuatia azimio namba mbili la wakuu wa vitengo wa madawa ya kulevya kutoka nchi washiriki uliofanyika Cairo nchini Misri mwezi Julai mwaka jana. Mwisho
|
| < Prev | Next > |
|---|