Main Menu
Useful Links
| Tahadhari za Usalama |
| Polisi Jamii |
| Vifungu vya Sheria |
| SMS & CALLS |
Who's Online
We have 4 guests onlineLogin Form
| WATATU WAFA NA WENGINE 12 KUJERUHIWA KATIKA AJALI ZA MAGARI |
|
TABORA JUMANNE MACHI 23, 2010 Watu watatu wamefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa vibaya katika ajali tatu tofauti za Barabarani zilizotokea jana katika mikoa ya Tabora, Shinyanga na Pwani.
Mkoani Tabora, mtu mmoja amefariki na wengine 12 kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyotokea kwenye barabara Kuu ya Igunga- Nzega mkoani humo.
Akizungumzia ajali hiyo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Tabora SSP Anthony Ruta, amesema kuwa ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 11.00 jioni kwenye kijiji cha Nanga eneo la Mlima Pasua katika Barabara ya Kuu ya Igunga-Nzega.
Amesema ajali hiyo imetokea baada ya Lori moja lenye namba za usajili T435 BCC likiwa na tela namba T 483 BBE likiendeshwa na Ali Ellye(35) kuigonga gari nyingine yenye namba T 489 AKY aina ya Isuzu Canter iliyokuwa ikiendeshwa na Salum Ali(32).
Kamanda Ruta amemtaja mtu mmoja aliefariki katika ajali hiyo kuwa ni utingo wa gari la Isuzu Rashidi Saidi(29), mkazi wa kijiji cha Mwisi Igunga mkoani Tabora.
Amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Kurwa Mohammedi(32) mfanyabiashara na kukazi wa Kijiji cha Simbo, Samweli Kuyeye(60) mkazi wa Nkinga, Lucas Mhindwa(29) wa Uswaya, Maduhu Shija(42) mkazi wa Mwisi, Charles Mahita(30) mkazi wa Simbo, Shija Kudelia(60) mkazi wa Mwisi.
Wengine waliojeruhiwa ni Salum Ali(32) mkazi wa Simbo ambaye ni dereva wa Canter na Joseph Makalanga(27) mkazi wa Uyuwi mjini Tabora, Michael Machibya(63) mkazi wa Kijiji cha Nkinga, Hassan Manua (23) mkazi wa Mwisi, Gilaya Butondo(30) mkazi wa Mwisi, Mabula Jackson(22) mkazi wa Meatu mkoani Shinyanga,
Kamanda Ruta amesema majeruhi wanne kati ya hao hali zao ni mbaya na wamelazwa katika Hospitali ya Misheni ya Nkinga wilayani Igunga kwa matibabu.
Amewataja majeruhi hao kuwa ni Michael Machibya(63) mkazi wa Kijiji cha Nkinga, Hassan Manua (23) mkazi wa Mwisi, Gilaya Butondo(30) mkazi wa Mwisi, Mabula Jackson(22) mkazi wa Meatu mkoani Shinyanga.
Huko mkoani Shinyanga, mtu mmoja aliyejulikana kwa jina moja amefariki dunia baada ya kugongwa na basi lenye nambari za usajili T. 326 AHB aina ya Scania mali ya Kampuni ya Mabasi ya KIMOTCO ya Mkoani Arusha lililokua likiendeshwa na Ali Azizi(38).
Kamnda wa Polisi mkoani Shinyanga ACP Daud Siasi, amemtaja marehemu kwa jina moja la Bi Paulina(50) ambaye ni mkazi wa Katoro Geita mkoani Mwanza.
Kamanda Siasi amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari hiyo lakini amesema tayari Polisi wanamshikilia Dereva wa basi hilo Ali Azizi(38) na atafikishwa mahakamani kujibu shitaka lake.
Huko Mkoani Pwani, mtu mmoja amefariki papohapo baada ya kugongwa na gari isiyofahamika huko kwenye maeneo ya Kiluvya katika Barabara Kuu ya Dar es Salaam- Morogoro.
Kamanda wa Polisi mkoani humo ACP Abousalom Mwakyoma, amemtaja marehemu kuwa ni Bi Monica William Mwanga(38) mkazi wa Kiluvya, ambaye mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Tumbi Kibaha mkoani humo.
Kamanda Mwakyoma ameseme Polisi wanamsaka dereva wa gari iliyosababisha ajaili hiyo ambayo inasadikiwa kuwa imetokana na mwendo kasi.
Mwisho |
| < Prev | Next > |
|---|