Main Menu
Useful Links
| Tahadhari za Usalama |
| Polisi Jamii |
| Vifungu vya Sheria |
| SMS & CALLS |
Who's Online
We have 9 guests onlineLogin Form
| IGP ATANGAZA MKAKATI WA KUPAMBANA NA RUSHWA KWENYE JESHI LA POLISI NCHINI |
|
SINGIDA JUMATANO, MACHI 03,2010. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, ametangaza mkakati wa kukomesha kabisa vitendo vya kudai na kupokea rushwa kama hatua ya kulinda heshma ya Askari na Jeshi hilo kwa ujumla. IGP Mwema ametangaza mkakati huo leo mjini Singida wakati wa mkutano wa Wadau kutoka Idara na Makampuni mbalimbali mkutano ambao uliongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Pastory Mabiti na askari Polisi wa vyeo mbalimbali. Amesema kuwa mkakati huo utasaidia kukomesha vitendo vya kudai na kupokea Rushwa na kuwakamata wale wote wanaowashawishi askari kupokea rushwa.
Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi amewaagiza askari kote nchini, kukataa vishawishi vya watu wanaotaka kuwapa rushwa na kwamba yeyote atakayekataa kupokea rushwa ya kiasi chochote cha fedha atamzawadi kiasi kama hichohicho kwa heshima ya kukataa rushwa. IGP Mwema ameongeza kuwa kula rushwa ili kuuza haki ya mtu ni dhambi na gharama ya askari kupokea rushwa ni kupoteza uwaminifu wake binafsi na wakati huo huo kulifanya Jeshi nalo lipoteze uaminifu wake kwa kwa wananchi. Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi nchini amesema kuwa Raia yeyote atakayethubutu kushawishi ama kutoa rushwa atakiona cha mtema kuni kwa vile atakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria kukabili shitaka lake lakini pia na kesi iliyokuwa ikimkabili na kupelekea kushawishi kutoa rushwa kwa askari.
Amesema Jeshi lake limetenga fedha za kutosha kukabiliana na wale wote watakaowashawishi askari kupokea rushwa. Tayari IGP amewaagiza makamanda wa Polisi wa mikoa na Vikosi nchini kote kuandaa orodha ya askari waliokataa kupokea rushwa katika kipindi cha kuanzia Januari mosi mwaka huu, ili waweze kuzawadiwa kiasi kile kile walichokataa kutoka kwa watoaji rushwa.
Kuhusu suala la ulinzi shirikishi, IGP Mwema amewapongeza wananchi wa mkoa wa Singipa kwa kujipanga vema katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu ukiwemo wa miundombinu ya mawasiliano na nishati ya umeme uliokuwa umekidhiri mkoani humo. Hata hivyo amepongeza juhudi na ushirikiano uliopo baina ya Jeshi la Polisi mkoani Singida na Wadau mbalimbali.
Wakati wa mkutano huo, wadau mbalimbali walielezea mipango yao kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoa wa Singida katika kukabili matukio ya kihalifu. maoni mazuri walioyatoa kupitia msanii wa mashairi Omari Yustin Gone kwamba kama rushwa ikiisha Jeshi la polisi, wananchi watatoa ushirikiano zaidi.
“Suala la ulinzi ni sehamu ya maisha yetu wenyewe, sisi wote tunashughulikia suala moja, na polisi peke yake haiwezi bila ushiriano wenu” alisema IGP. Wadau hao walikuwa wakitoa taarifa za utekelezaji wa vikosi kazi kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, ambaye yuko katika ziara ya kikazi ya wiki moja mkoani Singida.
Wadau waliotoa taarifa zao ni Katibu wa makampuni Binafsi ya Ulinzi Bw. Juma Sefu, Meneja wa NMB kwa niaba ya Muungano wa Mabenki mkoani Singida Bw. Lambileki Harodi, Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Singida Mchungaji Emmanuel Barnabas na Afisa Usalama wa Shirika la Umeme nchini Tanesco Bw. Lenin Kiobya. Wengine ni Meneja wa Kamupuni ya Simu TTCL Bw. Joseph Masangya, Kaimu Meneja wa TRA Bw. Lucas Mnabi, Katibu wa Chama cha Waganga na Wakunga wa Tiba Asililia, Mwakilishi wa Wazee wa Mkoa wa Singida Mzee Salim Najim pamoja na Wamiliki wa Makampuni binafsi ya Ulinzi mkoani humo na Viongozi wa Dini na Sumatra.
Akitoa taarifa ya hali ya uhalifu mkoani Singida, kamanda wa Polisi mkoani humo ACP Selina Kaluba, amesema kuwa uhalifu wa kuwania mali umepungua lakini kumekuwapo na ongezeko la makosa ya usalama barabarani. Amesema kuwa kuongezeka kwa makosa hayo kunatokana pia na misako inayofanywa na askari wa Kikosi cha Usalama barabarani kwa kushirikiana na askari wa vikosi vingine na wadau kama vile Sumatra na TRA. Makosa 8321 mwaka 2009 ikilinganishwa na makosa 7062 na kutozwa faini za papo kwa papo na jumla ya shilingi Milioni 316,250,000 zilipatikana ambapo shilingi 168,480,000 zilipatikana katika kipindi cha mwaka 2009 na shilingi 147,770,000 zilipatikana katika kipindi cha mwaka 2008 Mwisho
|
| < Prev | Next > |
|---|