Main Menu
Useful Links
| Tahadhari za Usalama |
| Polisi Jamii |
| Vifungu vya Sheria |
| SMS & CALLS |
Who's Online
We have 6 guests onlineLogin Form
| WATOTO WATATU RUKWA WAGONGWA NA GARI NA KUFARIKI DUNIA |
|
SUMBAWANGA RUKWA JUMANNE DESEMBA 08, 2009. Watoto watatu wakiwemo wawili wa familia moja wamefariki dunia na mwingine kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari jana huko kwenye kijiji cha Kisumba Barabara ya Matai- Kasanga mkoani Rukwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Jacobo Mwaruanda, amewataja watoto waliofariki kuwa ni Zawadi Simtowe(5), Mwanafunzi darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Kisumba na ndugu yake Edward Simtowe(1) na Paschal Mussa(12) Mwanafunzi, darasa la tatu shule ya Msingi ya Kisumba.
Amemtaja majeruhi ambaye amelazwa katika Hospitali ya Mkoa Sumbawanga kwa matibabu kuwa ni Ayoubu Clement(14), ambaye ni mwanafunzi, darasa la tano katika shule ya Msingi Kisumba.
Amesema kuwa ajali hiyo imetokea huko kwenye barabara ya Matai – Kasanga baada ya Lori lenye namba za usajili T.331 AMG aina ya Volvo baada ya kuacha njia na kuwagonga watoto hao waliokuwa wakitembea kwa miguu kandokando mwa barabara.
Amesema Polisi inamsaka Dereva aliyehusika katika ajali hiyo anayejulikana kwa jina moja la Koja ambaye alitoroka mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
WAKATI HUO HUO Polisi mkoani Rukwa wanamshikilia Mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi ya Kilimahewa wilayani Sumbawanga Joseph Katepa(30) kwa tuhuma za kumpa mimba mwanafunzi mmoja wa darasa la sita shuleni hapo mwenye umri wa mika 14. (Jina linahifadhiwa).
Mwalimu huyo anatuhumiwa kutenda kosa hilo katika vipindi tofauti tangu mwanzoni mwa mwezi September 2009 na kumpa ujauzito unaokadiriwa kuwa na miezi miwili sasa.
Amesema Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na watamfikisha mwalimu huyo mahakamani mara tu upelelezi kukamilika.
Mwisho |
| < Prev | Next > |
|---|