Main Menu
Useful Links
| Tahadhari za Usalama |
| Polisi Jamii |
| Vifungu vya Sheria |
| SMS & CALLS |
Who's Online
We have 7 guests onlineLogin Form
| TIMU YA TAIFA YA JESHI LA POLISI INAONDOKA LEO KWENDA MALAWI KUSHIRIKI MICHUANO YA SADC |
|
Timu ya Taifa ya Jeshi la Polisi nchini inayojumuisha wachezaji wa mpira wa miguu, Riadha na Dats, inaondoka nchini leo kwenda Blantyre nchini Malawi kwa ajili ya michuano ya michezo ya Majeshi ya Polisi kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC. Timu hiyo ambayo ina jumla ya wanamichezo 43 wakiwemo viongozi wawili inakwenda kushiriki kwa mara ya nne tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo mwaka 2003.
Akikabidhi Berera ya Jeshi la Polisi kwa Wachezaji hao, Mkuu wa Huduma za Polisi Jamii nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi Isaya Mngulu, amewataka wachezaji hao wakahakikishe kuwa wanashinda kwa kila mchezo ili kuleta sifa kwa Jeshi la Polisi na Taifa kwa ujumla.
Amewataka wakatangaze pia vivutio na Rasilimali za taifa tulizonazo kama vile Hifadhi zatu ukiwemo mlima wa Kilimanjaro na wanyama ili kuwavutia zaidi watalii na kuongeza uchumi wetu.
Awali Mkuu wa Michezo wa Jeshi la Polisi nchini ASP Jonas Mahanga, amesema tangu timu hiyo ianze kushiriki katika michuano hiyo, imekuwa mabingwa wa mchezo wa mpira wa miguu, Riadha na mara kwa mara wamekuwa mabingwa wa jumla na timi yenye nidhamu kuliko zote.
Hata hivyo amesema kuwa tofauti na miaka ya nyuma, mwaka huu timu hiyo inaondoka ikiwa na washiriki wachache ikilinganishwa na timu za majeshi ya Polisi kutoka nchi nyingine.
Amesema baadhi ya nchi zinapeleka wachezaji zaidi ya 200 kulingana na michezo wanayoshiriki lakini pia kutegemea na hali ya kiuchumi wa nchi husika.
Amesema kupeleka wachezaji wengi kunafaida kubwa kwa vile mara nyingi ubingwa wa jumla unatokana na idadi ya michezo na idadi ya medali na vikombe mtakavyovinyakua.
Hata hivyo amesema kuwa pamoja na uchache wao, watakwenda kuhakikisha kuwa wanashinda kwa kila mchezo ili kuleta sifa kwa Jeshi la Polisi na Taifa kwa ujumla.
Akizungumzia michuano hiyo, mmoja wa wanariadha maarufu nchini Francis Naali, ambaye ni Bingwa wa Jumuiya ya Madola wa mchezo huo, alisema kuwa anauhakuka wa kwenda kufanya vizuri zaidi.
Jumla ya nchi 12 zinatarajia kupeleka wachezaji wake katika michuano hiyo huku kila mmoja ikitegemea kushinda na kuchukua ubingwa kwa kila mchezo.
Michuano hiyo ambayo hufanyika kila baada ya mwaka moja ilianza mwaka 2003 nchini Afrika ya Kusini, 2005 ilifanyika nchini Botswana na 2007 ilifanyika nchini Zimbabwe na Jeshi la Polisi hapa nchini limewahi kuwa bingwa wa mpira wa miguu mara mbili mfululizo.
Nchi zitakazoshiriki katika michuano hiyo ni Angola. Afrika ya Kusini, Botswana, Msumbiji, Lesotho, Swaziland, Zambia, Zimbabwe, Tanzania, DRC Congo na wenyeji Malawi.
Mwisho
|