|
MUUNDO WA JESHI LA POLISI
Baada ya Uhuru majukumu makubwa ya Jeshi la Polisi ni kulinda raia na mali zake Tanzania visiwani na Tanzania bara na si kulinda kundi la watu wachache kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni
Awamu zote tatu za utawala ya serikali hapa nchini, Jeshi la Polisi lilikuwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani na serikali ya awamu ya nne ikaamua kuunda Wizara ya Usalama wa Raia ambapo Jeshi la Polisi liliondolewa Wizara ya Mambo ya Ndani na kuhamishiwa ya Wizara ya Usalama wa Raia mwaka 2006.
Jeshi la Polisi linaongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IJP) akisaidiwa na Makamishna watano:-
Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ambaye atakuwa na majukumu ya kusimamia usalama wa raia katika Jiji la Dar es Salaam ambalo limegawanywa katika mikoa mitatu ya Kipolisi ambayoi ni Ilala, Temeke na Kinondoni.
Kamishna wa Utawala na Fedha ambaye anashughulikia utawala na fedha katika Jeshi la Polisi na anakuwa msimamizi mkuu katika masuala ya ukaguzi, mipango na maendeleo ya Jeshi.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo anakuwa msimamizi mkuu wa masuala ya mafunzo na operesheni katika idara na vitengo mbalimbali vya Jeshi la Polisi kama vile Reli, Tazara na Kikosi cha Wanamaji na kadhalika. Pia anashughulikia Mahusiano ya Jeshi la Polisi na vyombo vya habari, Michezo, Bendi, kikosi cha Kuzuia Uhalifu, Mgambo na Polisi jamii.
Kamishna wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ambaye anakuwa mkuu wa masuala yote yanayohusu makosa ya Jinai.
Kamishna wa Polisi Zanzibar ambaye jukumu lake kuu ni kusimamia kazi za Polisi visiwani Zanzibar.
Makamishna wote hao wanasaidiwa na Maofisa Wasaidizi na Waandamizi wa Jeshi la Polisi katika kazi zao za kila siku.
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi yapo jijini Dar es Salaam na kila mkoa hapa nchini kuna Kamanda wa Polisi wa Mkoa ambaye anawajibika moja kwa moja kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na kila mkoa kuna Wakuu wa Polisi wa Wilaya wenye majukumu ya kusimamia shughuli za kila siku za Utawala na Kijeshi katika Wilaya husika.
VITENGO ZAIDI VYA JESHI LA POLISI
Kuna vitengo mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi ambavyo vinasaidia kusukuma mbele kazi za polisi na vitengo
|