Wajerumani walifika Tanganyika ili kutawala, waliunda kikundi cha watu kilichofanya kazi ya Polisi.
1916
Vita kuu ya kwanza ikiendelea Ulaya na Afrika, kundi la Maafisa 31 (NCO) kutoka Afrika Kusini wakiwa na silaha (Rifle) walifika Tanganyika kufanya kazi za Polisi.
1919
Tarehe 25 August 1919 Serikali ya Kiingereza ilitangaza katika Gazeti la Serikali No.Vol.1 No.21-2583 kuwa Jeshi la Polisi Tanganyika limeanzishwa rasmi. Makao Makuu ya Jeshi hilo yalikuwa Wilayani Lushoto chini ya uongozi wa Major S.T DAVIS.
1921
Kundi lingine la Wakaguzi kutoka Ulaya lilifika nchini Tanganyika kuanzisha shule ya Mafunzo ya Polisi huko Morogoro.
1925
Kituo cha kwanza rasmi cha Polisi nchini kilifunguliwa huko Lupa Tingatinga kwenye machimbo ya dhahabu Chunya.
1930
Makao Makuu ya Polisi yalihamishwa kutoka Lushoto kuja Dar es Salaam.
1949
Motorized Company sasa Field Force Unit (F.F.U) kilianzishwa nchini kurejesha amani penye vurugu.
1949
Vijana mbalimbali wa Kiafrika toka shule mbalimbali za Sekondari Nchini walichaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi na kuwa Wakaguzi chini ya uangalizi (Probation Inspectors).
1952
Kikosi cha Mawasiliano (Signals Branch) kilianzishwa katika Polisi bila kutumia nyaya za simu.
1958
Askari wa Polisi wa Kikie (Women Police) walijiunga na Jeshi la Polisi chini ya uongozi wa Miss. Payee.
1961
Tarehe 9 Desemba, 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake. Baada ya uhuru, Jeshi la Polisi lilianza kubadili mwelekeo toka katika kutumikia Wakoloni na Walengwa wakawa ni Wananchi kwa mujibu wa sera za Serikali ya Wananchi.
1962
Kwa mara ya kwanza nafasi ya Kamishna wa Polisi aliyekuwa Mzungu Mr. M.S Wilson – C.P, ilichukuliwa na Mwafrika
Mr. Elangwa Shaidi – C.P.
1962
Maafisa 10 Waafrika waliteuliwa kuchukua nafasi za wakuu wa Polisi wa Mikoa (Regional Police Commanders).
1964
Tarehe 26/04/1964 Tanganyika na Zanzibar ziliungana na hivyo kuunda Tanzania. Kwa hiyo Mr. Elangwa Shaidi alipandishwa cheo nakuwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IJP).
Alisaidiwa na Makamishna watatu wa Polisi ambao ni:-
1.
Mr Edington Kisasi
Kamishna wa Polisi Zanzibar.
2.
Mr. Hamza Azizi
Kamishna wa Polisi Bara.
3.
Mr. Akena
Kamishna wa Polisi CID.
VIONGOZI WA JESHI LA POLISI WAKATI WA UKOLONI HADI UHURU.
1916 – 1920
Major S.T. Davis.
1920 – 1929
E.F. Brown.
1929 – 1933
G.H. Kiram.
1933 – 1942
F.A.B. Nicholl.
1942 – 1949
E.B. Birthray.
1949 – 1951
W.A. Muller.
1951 – 1958
R.E. Fouler.
1958 – 1962
G.S. Wilson.
1962 – 1964
E.N. Shaidi.
INSPEKTA JENERALI WA POLISI TANGU MUUNGANO HADI LEO.
1964 – 1970
1970 – 1973
Elangwa N. Shaidi
Hamza Azizi.
7/8/1973 – Aug 1975
8/8/1975 – Nov 1980
Samweli H. Pundugu.
Philemon N. Mgaya.
2/11/1980 – 30/11/1984
1/12/1984 – 3/5/1996
Solomoni Liani.
Harun G. Mahundi.
4/5/1996 – 2/3/2006
3/3/2006 Hadi sasa
Omar I. Mahita.
Saidi A. Mwema.
WAKURUGENZI WA IDARA YA UPELELEZI (CID) TANGU 1960 HADI LEO.