Wahalifu

MAGENI S/O MUSOBI @ JOHN MMANUEL KUSIHA Hii ni sura ya mhalifu anaetafutwa kwa kosa la wizi wa mamillioni ya fedha hapa nchini. Inasadikiwa kukimbilia Bangalore India.  

KATILAL S/O RANA Hii ni sura ya mhalifu anaetafutwa kwa kosa la wizi wa mamillioni ya fedha hapa nchini. Inasadikiwa kukimbilia New Dehli - India

     

SHINYANGA, kwa wizi akiwa mtumishi, WILLIAM S/O SALAMBA, MUSA SALAMBA AU CHAGULA CHAGULA, mwanaume, msukuma, miaka 43, urefu wake futi 5 inchi 7, macho meusi, nywele fupi, anapendelea kunywa pombe aina ya Kilimanjaro.

Muhasibu. Kwa mara ya mwisho alionekana amevaa suruali na shati la maua mikono mirefu, Mara kwa mara hutembelea MWANZA, SHINYANGA, DAR ES SALAAM NA KAMPALA UGANDA, Kwa kawaida hukaa Kijiji cha Mondo, Wilaya ya Kishapu. (kumb: SHY/IR/4160/2005).

 

KIGAMBONI, kwa Wizi wa silaha,- 

 

 

 

SAIDI S/O MSUMCHE au NATHANAEL, Mwanaume, Mgogo,Mweupe, Miaka 19, Urefu futi 5 na inchi 4, sura ya mviringo, shingo ndefu.Msera wa kijiweni.

kwa mara ya mwisho alionekana amevaa jeans nyeusi na Tshirt ya Blue, pia alikuwa amesuka nywele, kwao ni Serengeti Kigamboni, (kumb: KGD/RB/141/2006).

     
 Wizi wa silaha,- BENJAMINI PETRUS NGAYALINA, Mwanaume, miaka 20, Mweusi,Mnyamwezi, Urefu futi 5 na inchi 6, Jicho la kulia halina nguvu ya kupanuka sana anapoangalia, sura ndefu.Mwanafunzi wa Navy Sec School Kigamboni. kwa mara ya mwisho alionekana amevaa suruali ya jeans na Tshirt Nyekundu yenye fito ya Blue shingoni. Kwao ni kwa Chagani Kigamboni. (kumb: KGD/IR/141/2006)    Utoro Jeshini,- E.9291 D/C FRANK MBUTU, Mwanaume,Miaka 33, Urefu futi 5 na inchi 8, Uso wa mviringo.Askari Polisi. kwa mara ya mwisho alionekana amevaa suruali ya kawaida na shati la mikono mifupi, Hupenda kutembelea miji Mpwapwa na Dar es salaam. Kwao ni Singida Mjini. (kumb: OB/IR/670/2006).
     
Kutoka OYSTERBAY, kwa Mauaji, - D.901 D/SSGT JAMES MASOTA, Mwanaume, Miaka 46, Futi 5 na inchi 10, Mweusi, Uso wa mviringo.Askari Polisi. kwa mara ya mwisho alionekana amevaa suruali ya kawaida na shati la mikono mirefu. Hupenda kutembelea Mwanza mjini, kwao ni Magu. (kumb: OB/IR/670/2006)   Kutoka OYSTERBAY, kwa Mauaji D.4656 D/CPL RAJABU BAKARI Mwanaume, Myao, miaka 42, urefu futi 5 inchi 6, ana kovu bega la kulia, maji ya kunde, mpole, hupendelea kutaba samu wakati anapoongea.Askari Polisi. Kwa mara ya mwisho alionekana amevaa shati na suruali ya kawaida, mara kwa mara hutembelea DAR ES SALAAM, LINDI NA MTWARA. Kwa kawaida hukaa Kijiji cha Muungo Wilaya ya Masasi. (kumb: OB/IR/670/2006).
     
Kutoka OYSTERBAY, Kwa mauaji D. 5682 DC SAAD, Mwanaume, Mluguru, miaka 43, urefu 5 inchi 10, maji ya kunde, uso wa mviringo.Askari polisi. Mara ya mwisho alionekana amevaa suruali ya jeans na T-shirt. Mara kwa mara hutembelea TANGA, DAR ES SALAAM NA MOROGORO, Kwa kawaida hukaa Kijiji cha Kitope Wilaya ya Ifakara. (kumb: 0B/IR/670/2006).   Kutoka MAKAO MAKUU POLISI DSM, Mwanamke mweupe (mwarabu) mfupi uso wa mviringo na ana chunusi nyingi usoni kazi uuzaji wa viwanjaHii ni sura ya mhalifu anaetafutwa kwa Kwa kosa la kughushi nyaraka na kuiba fedha kwa njia ya udanganyifu. umri wake ni kati ya miaka 40 – 45 anapendelea kuvaa baibui Mara kwa mara hutembelea TANGA, DAR ES SALAAM NA ZANZIBAR kumb:CD/IR/5266/2006.

Copyright 2010 Tanzania Police Force Website.