Forensic

 

Ofisi ya Forensic Bureau Dar es Salaam ni mojawapo ya vitengo vya ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi
wa Jinai Nchini.Ofisi hii hutoa huduma mbalimbali za uchunguzi wa maabara ya Makosa ya Jinai,
sambamba na kazi ya uchunguzi wa Kitaalam, ofisi hii pia hutoa huduma kwa watu binafsi, mashirika ya Umma, Idara mbalimbali za umma, Serikali, Makampuni ya Ulinzi Balozi mbalimbali zilizopo hapa Nchini na nje ya Nchi, Benki, BOT, NMB, NBC n.k.

Zifuatazo ni gharama na huduma zinazotolewa katika ofisi hii

S/No 
 
AINA YA HUDUMA
GHARAMA ZA UCHUNGUZI
1.
Hati ya Tabia Njema (Police Clearance Certificate/certificate of good conduct).
  • Tsh 2000/= kwa waombaji ambao ni Raia wa
  • Tanzania wanaoishi Nchini tu.
  • US$ 25/= au sterling Pound 15/=
  • kwa Raia wa kigeni ambao sio watanzani.
  • US$ 25/= au sterling Pound 15/= kwa Raia wa
  • Tanzania ambao wanaishi nje ya nchi watawajibika
  • kutuma alama za vidole kutoka Nchi wanazoishi na
  • kuzileta Forensic Bureau Dar es Salaam
2.
Maombi ya uraia wa Tanzania (Citizenship)
  • US$ 25/= au sterling Pounds 15/=
3.
Watu wanaoajiriwa na Makampuni Binafsi, Idara za Serikali, Mashirika ya Umma, Mabenki Kampuni za Ulinzi, n.k.
  • TSh. 2000/= kwa waajiriwa ambao ni watanzania
  • US$ 25/= au sterling Pound 15/=
  • Kwa Raia wa kigeni wanaotaka kuajiriwa Nchini.
4.
Uchunguzi wa Hati mbalimbali na kesi zisizopitia Polisi ambazo zimeletwa kupitia kwa wakili.
  • Hati halisi inayobishaniwa
  • Vielelezo specimen vya
    watuhumiwa
    (Requested specimen)
  • Barua (covering letter) vielelezo.
  • Malipo ya chini (minimum) fee ni TSh 50,000/=
    kwa kesi moja.
  • Gharama ya uchunguzi itaongezeka kutegemeana na wingi
  • wa vielelezo.
5.
Uchunguzi wa Magari (Vehicle Inspection report) magari ambayo hufanyiwa uchunguzi na kitengo cha Polisi Interpol Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam.
  • TSh 5,000/= kwa gari moja.
Kwa Maelekezo zaidi fika katika Ofisi yeyote ya Polisi Mkoani au watumie S.L.P 9094 Maabara ya uchunguzi (Forensic Bureau) Dsm. au Tumia e mailphq@policeforce.go.tz

 

 

Copyright 2010 Tanzania Police Force Website.