|
USALAMA WA RAIASAVINGS AND CREDIT COOPERATIVE SOCIETY LIMITED
{Kwa Ustawi na Usalama}
1. UTANGULIZI
URA SACCOS LTD ni ushirika wa Akiba na Mikopo ulioanzishwa kwa ajili ya Watumishi wa Jeshi la Polisi Tanzania pamoja na Familia zao.
Ushirika huu ulisajiliwa mnamo tarehe 06 Septemba, 2006 na kupata namba ya usajili DSR 904.
Ushirika huu ulizinduliwa na Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya M. Kikwete mnamo tarehe 09 Septemba, 2006 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar Es Salaam.
2. JUKUMU LETU
Kutoa huduma bora za kifedha kwa masharti nafuu yanayokidhi mahitaji ya wanachama na wateja.
3. LENGO LETU
Kuwa Asasi ya huduma za kifedha iliyoendelevu yenye mtandao wa kitaifa na yenye uwezo mkubwa wa kuboresha hali ya kiuchumi ya watumishi wa Jeshi la Polisi na Familia zao.
4. SIFA ZA KUWA MWANACHAMA
Awe ni askari Polisi au Mtumishi raia wa Jeshi la Polisi,
Awe sehemu ya familia ya Mtumishi wa Jeshi la Polisi Tanzania,
Awe amelipa kiingilio cha shilingi 5,000/= kiwango kinaweza kubadilika,
Awe amenunua hisa 20 kwa shilingi 5,000 kila moja (jumla shilingi laki moja 100,000 kiwango kinachoweza kubadilika,
Awe ameridhia kuchangia akiba isiyopungua shilingi 10,000/ kila mwezi,
Awe tayari kufuata sheria ya Vyama vya Ushirika Na.20/2003 na marekebisho yake wakati wowote na kufuata na kuheshimu Masharti na sera za URA SACCOS Ltd.
5. FAIDA ZA KUWA MWANACHAMA
Kuwa mmoja wa wamiliki wa Ushirika huu,
Kuwa na haki ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa Kiongozi katika Ushirika,
Kupata fursa ya kuwekeza katika kununua hisa na kupata gawio la faida,
Kutumia na kupata huduma ya akiba, amana na mikopo,
Kupata elimu ya ujasiriamali n.k
6. BIHAA NA HUDUMA ZINAZOTOLEWA
01. HISA
Hisa huwakilisha sehemu ya umiliki wa Ushirika (wingi wa hisa ndio ukubwa wa umiliki),
Mwanahisa anayohaki kwenye mali yeyote ambayo ushirika unamiliki,
Mwanahisa anahaki ya kupata gawio kutoka kwenye faida kwa kiwango kilichoamriwa kigawiwe kwenye Mkutano Mkuu,
Mwanahisa anaweza kupata faida kama thamani ya hisa itapanda,
Mwanahisa anahaki ya kupiga kura kwenye Mkutano Mkuu wa Chama kulingana na taratibu za chama.
0.2 AKIBA
Hii ni michango ambayo Mwanachama anajiwekea katika Akaunti yake mara kwa mara kwa ajili ya kukidhi mahitaji yake ya baadaye kadri ya uwezo wake.Mwanachama anaweza kujiwekea michango hii kutoka kwenye Mshahara au Fedha taslim.
SIFA NA FAIDA ZA AKIBA
Haina gharama ya uendeshaji kwa Mwanachama,
Huduma hii humuwezesha Mwanachama kufikia lengo sababu Mwanachama huweza kuweka pesa yake kidogo kidogo kwa muda mrefu.
Humuwezesha mteja kukopa hadi mara tatu ya akiba aliyojiwekea kwa kuzingatia kanuni za mikopo.
Huduma hii humuwezesha Mwanachama kujenga tabia ya kujiwekea mara kwa mara [saving culture]
0.3 AMANA
AMANA YA MALEZI BORA
Hii ni Akaunti ambayo Mzazi/Mlezi anajijengea uwezo wa kumudu mahitaji ya mtoto kutokana na mapato yake mwenyewe, mahitaji hayo yanaweza kuwa ada za shule, sare, vifaa vingine vya elimun.k.
SIFA NA FAIDA ZAKE
Ni akaunti ya motto mwenye umri usiozidi miaka 18 kwa usimamizi wa mzazi/mlezi
Mzazi/Mlezi anaweza kuweka pesa kwa njia ya makato toka katika mshahara au pesa taslimu,
Faida/Riba nzuri itatolewa katika amana inayozidi shilingi 50,000/
Fedha hutolewa mara 2 tu kwa mwaka na sio zaidi ya hapo,
Kiwango kisichopunguwa shilingi 10,000/ kitapaswa kuwekwa kila mwezi,
AMANA YA KAWAIDA
Ni mfumo wa kujiwekea pesa kwa ajili ya kukidhi haja mbalimbali wakati wowote.
SIFA NA FAIDA ZAKE
Mwanachama yeyote anaweza akatumia huduma hii, kwa udhamini wa wanachama wenzake wawili,
Mwanachama anaweza kuchukuwa pesa kutoka kwenye akaunti hii wakati wowote
Atapata kiwango kizuri cha riba kutegemeana na wakati husika
AMANAYA MALENGO MAALUM[Jipange Akaunti]
Ni mfumo wa kujiwekea pesa kwa ajili ya malengo maalum mfano likizo au kujikimu kimaisha wakati mfanyakazi akisubiri mafao yake baada ya kustahafu.
Sifa na Faida zake
Mwanachama yeyote anaweza kutumia huduma hii,
Mwanachama anaweza kuweka pesa zake kwa njia ya mshahara au pesa tasilimu,
Mwanachama anaweza kuchukuwa pesa kutoka kwenye akaunti hii katika tarehe aliyoitaja awali,
Kiwango kizuri cha riba kitatolewa kutegemeana na wakati husika,
AMANA YA MUDA MAALUM [fixed deposit account]
Ni mfumo wa kujiwekea pesa kwa kipindi Fulani ili kukidhi malengo ya wakati huo[mfano kwa miezi 3,6,9,12].
Sifa na Faida zake
Mwanachama yeyote anaweza kutumia huduma hii kwa kiwango kinachoanzia Tshs 200,000/=
Inakupa fursa ya kujua faida [riba] utakayopata,
Mwanachama haruhusiwi kuchukuwa pesa hadi pale muda wa makubaliano utakapofika,
Hati maalum itatolewa kuthibitisha umiliki wa amana hii.
0.4 MIKOPO
Mikopo ya dharura
Hii ni mikopo ambayo hutolewa kwa ajili ya kukidhi dharura za wanachama kwa mfano matibabu, mazishi n.k
Mkopo hutolewa ndani ya saa 12 za kazi baada ya maombi kupokelewa,
Mkopo huu hauzidi kiasi cha shilingi 500,000/ tu kwa muda wa marejesho usiozidi miezi 6
Mwombaji inabidi aoneshe viambatanisho vya dharura na sio vinginevyo
Mikopo ya Elimu (Elimika)
Hii ni mikopo kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya elimu kwa wakati, mfano ada, sare n k.
Mkopo huu hauzidi kiwango cha shilingi 1,000,000/ kwa muda wa marejesho usiozidi miezi 12.
Mkopaji atatakiwa kuambatanisha mchanganuo wa malipo kutoka taasisi husika pamoja na akaunti ya shule husika kwa kuwa pesa zitalipwa moja kwa moja shuleni.
Mikopo ya rasilimali za ujenzi[duty free shops]
Hii ni mikopo maalum kwa ajili ya kununua vifaa vyenye msamaha wa kodi katika maduka ya Polisi yenye misamaha ya kodi kwa mfano saruji, bati, nondo n.k
Mikopo hii itatolewa kulingana na gharama za bidhaa ambazo mwanachama anahitaji,
Muda wa marejesho ni ndani ya miezi 36,
Mikopo ya Wajasiriamali
Hii ni mikopo maalum kwa ajili ya kuendeleza shughuli za miradi ya uzalishaji mali inayotambulika kisheria,
Ni fursa ya kuongeza kipato na kupunguza ukali wa maisha,
Mkopaji atatakiwa kuwasilisha mchanganuo wa mradi husika,
Mwombaji atatakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao ni wanachama wa URA SACCOS Ltd
Kiwango cha mkopo hakitozidi mara tatu ya akiba za mwombaji zilizokaa chamani miezi mitatu,
Kwa mkopaji wa mara ya kwanza kiwango cha mkopo hakitozidi shilingi milioni 10 na mkopo wa pili hautatolewa ndani ya miezi 6 baada ya mkopo wa kwanza kutolewa,
Muda wa marejesho hautazidi miaka 3,
Kwa kiwango cha mkopo kinachozidi shilingi milioni 10, dhamana itahitajika ambapo mwenza[mke au mume] atahitajika ahusishwe kama mali husika ni ya familia.
Mkopo wa uwiano wa mshahara
Ni mkopo wenye masharti nafuu kwa wanachama ambao ni watumishi tu,
Kiwango cha mkopo kitategemea mahitaji ya mwanachama na uwezo wake wa kufanya marejesho katika mshahara bila kuathiri sheria za kazi,
Wanachama wanaotoroka kazi wakiwa bado wanadaiwa watafuatiliwa huko walipo ili walipe madeni na ikishindikana basi mafao yao ya GEPF au PSPF yatazuiliwa wakati hatua za kisheria zinachukuliwa.
Mikopo ya wanafamilia
Hii ni mikopo kwa ajili ya mume/mke na mtoto wa mtumishi wa jeshi la Polisi ambaye ni mwanachama wa URA SACCOS na mwenye shuguli inayomletea kipato halali,
Elimu ya awali juu ya matumizi bora ya mkopo itatolewa kwa mwanachama,
Ni fursa ya kuongeza kipato ndani ya familia kumudu mahitaji mbalimbali,
Mkopo hautazidi mara 3 ya akiba ya mwanachama iliyokaa zaidi ya miezi 3 kwenye chama,
Kiwango cha juu cha mkopo kwa mwanafamilia hakitazidi shilingi milioni 10,
Wadhamini wawili ambao wote ni wanachama wa URA SACCOS akiwemo yule ambaye mwanafamilia anatoka,
NB Pale ambapo afisa mikopo ataona inafaa atashauri uwepo wa dhamana ya mali.
05. SMS BANKING [Ujumbe mfupi wa maneno]
Hii ni huduma ya kuwawezesha wanachama kupata taarifa za kibenki na huduma zingine za kibenki kwa kupitia ujumbe mfupi wa maneno kwa kutumia simu za mkononi.
Mwanachama popote pale na muda wowote alipo anaweza kupata kujua salio lake kwenye akaunti yake ya akiba, amana, n.k
Mwanachama pia anaweza kupata taarifa mbalimbali za Chama kama vile Mkutano Mkuu, kujua kama amekubaliwa kupata/kukataliwa mkopo alioomba n.k
Gharama nafuu itatozwa kwa kila ujumbe utakaotumwa,
Kila mwanachama atapewa namba ya siri inayostahili kutunzwa na mwanachama mwenyewe.
06. ATM [Tembo Card SACCOS]
Hii ni huduma ambayo itamwezesha mwanachama kuchukuwa pesa tasilimu kutoka kwenye mashine za kuchukulia pesa bila kuhitajika kufika kwenye ofisi za URA SACCOS,
Sehemu yeyote ile ambayo mwanachama atakuwepo, muhimu tu kuwe na ATM za CRDB au VISA atapata huduma hiyo,
Muda wowote mwanachama anaweza kupata huduma kwa fedha zake zilizopo URA SACCOS
Hivyo, huduma hii itapunguza usumbufu kwa wanachama wake wa maeneo mbalimbali kupata pesa zao za mikopo amana n.k
Kwa maelezo zaidi, wasiliana nasi kwa:
URA SACCOS LIMITED
S.L.P. 46388 Dar Es Salaam
Simu:+255 732 921 481
Nukushi:+255 22 2850068
Barabara ya Kilwa, Temeke
Dar Es Salaam-Tanzania [E.A]
|