Home

SARPCCO1

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Said Mwema akipokea Kitara kutoka kwa Kamishna wa Jeshi la Polisi Nchini Afrika Kusini Mangwashi Phyega kama ishara ya kukabidhiwa Uenyekiti wa Wakuu wa Polisi kwa Nchi za Kusini Mwa Afrika (SARPCCO) .

POLISI NA MATUKIO

  • Waarabu sita wakamatwa Arusha Open or Close

    Walikuwa njiani kutoroka kupitia mpaka wa Namanga.FBI watua kuchunguza. Jeshi la Polisi mkoani Arusha , linawashikilia kwa mahojiano watu wenye asili ya kiarabu wanaotuhumiwa kulipua bomu kanisa katoliki jijini Arusha na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine 59 kujeruhiwa. Kwa upande mwingine askari wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), wamewasili mjini Arusha jana asubuhi kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kuwasaka watu waliohusika na mlipuko wa bomu katika kanisa la Parokia ya Joseph Mfanyakazi Olasite.

  • Taifa liyakatae matamshi ya uchochezi Open or Close

    Maoni ya Mhariri, anasema kuwa kufuatia kauli iliyotolewa na Mbunge wa Iramba Mashariki, Tundu Lissu, kwamba katika tukio la bomu jijini Arusha, serikali ndiyo inapaswa kulaumiwa kwa vile ndiyo chanzo cha chokochoko za udini nchini, kauli ambayo imelaaniwa vikali na haikupaswa kutolewa hasa kwa kiongozi kama yeye kutokana na kauli hiyo kutokuwa na lengo la kuchangia au kusaidia kutafuta ufumbuzi wa tatizo bali kuzidisha tatizo lenyewe

  • Mbaroni kwa kukutwa na mikia ya tembo Open or Close

    Watu watano wanashikiriwa mkoani Ruvuma kwa tuhuma mbalimbali za uhalifu likiwamo la kukutwa na risasi pamoja na mikia miwili ya tembo.

  • Polisi yasisitiza utii wa sheria bila shuruti Open or Close

    Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Matenga, kata ya Ikuwo, wilayani Makete wametakiwa kuelewa dhana ya utii wa sheria bila shuruti inayotekelezwa na Jeshi la Polisi nchini ili kuondokana na athari zinazotokana na kukaidi kutii sheria.

  • Polisi wakamata kilo 178 za bangi , kilo 52 za mirungi Open or Close

    Kamanda wa Polisi mkoani Tanga Costantine Massawe, amewataka watu wanaojihusisha na biashara za dawa za kulevya, kuwaonea huruma wakazi wenzao wa Jiji la Tanga kutokana na madhara ya kiafya wanayoyapata baada ya kujiingiza kwenye matumizi yake. Ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya kukamata kilo 178 za bangi na kilo 52 za mirungi kwa waandishi wa habari mkoani humo.

  • Jalada la Lwakatare kwa DPP Open or Close

    Upelelezi wa kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wifred Lwakatare na Ludovick Joseph, umekamilika na jalada lake litapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kwa hatua zaidi.

  • Polisi wakusanya milioni 825 makosa barabarani Open or Close

     Jeshi la Polisi mkoani Pwani limefanikiwa kukusanya kiasi cha zaidi ya Shilingi Milioni 825 kutokana na makosa madogo madogo ya barabarani kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

  • Ushiriki wananchi Polisi Jamii umeleta mafanikio Open or Close

    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mwinyihaji Makame amesema ushiriki wa wananchi katika Ulinzi Shirikishi kupitia Polisi Jamii umeleta mafanikio katika kupunguza vitendo vya uhalifu nchini

 

We have 41 guests and no members online