• Mwombaji anatakiwa kuwa na leseni ya Udereva ya daraja lolote lile iliyo hai ya hapa Nchini.
  • Anatakiwa kuipeleka leseni yake ofisi ya Mamlaka ya Leseni (T) TRA kwa ajili ya ukaguzi,
  • Baada ya Ukaguzi, Mamlaka ya Leseni (T) TRA itatoa barua rasmi kwenda kwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani(T) kuthibitisha uhalali wa leseni hiyo.
  • Ofisi ya Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (T) itakagua leseni hiyo pamoja na cheti cha Umahiri (Certificate of Competence) kuthibitisha uhalali wa leseni na cheti hicho cha umahiri.
  • Baada ya kuthibitisha uhalali wa leseni hiyo, Ofisi ya Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (T) itatoa barua rasmi kwenda Oisi ya Automobile Association Tanzania ambayo ndiyo asasi pekee hapa nchini yenye Mamlaka ya kutoa leseni za Kimataifa.