Saturday, May 19, 2012

Mgeni rasmi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Said Mwema akikata utepe kuzindua huduma ya X-ray katika Hospitali kuu ya Polisi iliyopo barabara ya kilwa, kurasini jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Said Mwema akikagua machine ya miozi (x-ray) mara baada ya kuzindua huduma hiyo katika hospitali kuu ya Polisi barabara ya kilwa kurasini jijini Dare s salaam.

Kikundi cha sanaa cha Jeshi la Polisi kikitumbuiza kusherehesha hafla ya uzinduzi wa huduma ya x-ray katika hospitali kuu ya Polisi barabara ya kilwa kurasini jijini Dar es salaam

Leseni ya kimataifa

UTARATIBU WA KUPATA – INTERNATIONAL DRIVING  PERMIT

HAPA NCHINI.

  • Mwombaji anatakiwa kuwa na leseni ya Udereva ya daraja lolote lile iliyo hai ya hapa Nchini.
  • Anatakiwa kuipeleka leseni yake ofisi ya Mamlaka ya Leseni (T) TRA kwa ajili ya ukaguzi,
  • Baada ya Ukaguzi, Mamlaka ya Leseni (T) TRA itatoa barua rasmi kwenda kwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani(T) kuthibitisha uhalali wa leseni hiyo.
  • Ofisi ya Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (T) itakagua leseni hiyo pamoja na cheti cha Umahiri (Certificate of Competence) kuthibitisha uhalali wa leseni na cheti hicho cha umahiri.
  • Baada ya kuthibitisha uhalali wa leseni hiyo, Ofisi ya Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (T)  itatoa barua rasmi kwenda Oisi ya Automobile Association Tanzania ambayo ndiyo asasi pekee hapa nchini yenye Mamlaka ya kutoa leseni za Kimataifa.