Thursday, February 23, 2012
Serikali ya Japan yatoa msaada kwa serikali ya Tanzania

Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya mambo ya ndani imepokea Msaada wa magari 11 aina ya Toyota landcruiser na boti 3 kutoka kwa serikali ya Japani kwa ajili ya kufanyia doria za kukamata wahamiaji haramu hapa nchini.

 

Msaada huo ulipokelewa na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mhe.Shamsi vuai Nohodha kwa niaba ya serikali ya Tanzania ambapo amesema magari matano na boti 3 watapatiwa Jeshi la Polisi na magari sita watapatiwa Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya kufanya doria.

Naye Balozi wa Japani nchini Tanzania, Bw. Masaki Okada amesema serikali ya Japani imetoa msaada huo wa magari 11 na boti 3 kwa Jeshi la Polisi na Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya kufanyia doria hasa katika Mikoa ya Lindi, Mbeya, Mtwara pamoja na Mkoa wa Tanga.