Haya ni mabwalo ya police ambayo yanatumika katika sherehe nyingi za kipolisi na kijamii.
1. Police college gym
2. Police officers mess Gym
3. Ukonga Gym
Walikuwa njiani kutoroka kupitia mpaka wa Namanga.FBI watua kuchunguza. Jeshi la Polisi mkoani Arusha , linawashikilia kwa mahojiano watu wenye asili ya kiarabu wanaotuhumiwa kulipua bomu kanisa katoliki jijini Arusha na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine 59 kujeruhiwa. Kwa upande mwingine askari wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), wamewasili mjini Arusha jana asubuhi kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kuwasaka watu waliohusika na mlipuko wa bomu katika kanisa la Parokia ya Joseph Mfanyakazi Olasite.
Maoni ya Mhariri, anasema kuwa kufuatia kauli iliyotolewa na Mbunge wa Iramba Mashariki, Tundu Lissu, kwamba katika tukio la bomu jijini Arusha, serikali ndiyo inapaswa kulaumiwa kwa vile ndiyo chanzo cha chokochoko za udini nchini, kauli ambayo imelaaniwa vikali na haikupaswa kutolewa hasa kwa kiongozi kama yeye kutokana na kauli hiyo kutokuwa na lengo la kuchangia au kusaidia kutafuta ufumbuzi wa tatizo bali kuzidisha tatizo lenyewe
Watu watano wanashikiriwa mkoani Ruvuma kwa tuhuma mbalimbali za uhalifu likiwamo la kukutwa na risasi pamoja na mikia miwili ya tembo.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Matenga, kata ya Ikuwo, wilayani Makete wametakiwa kuelewa dhana ya utii wa sheria bila shuruti inayotekelezwa na Jeshi la Polisi nchini ili kuondokana na athari zinazotokana na kukaidi kutii sheria.
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga Costantine Massawe, amewataka watu wanaojihusisha na biashara za dawa za kulevya, kuwaonea huruma wakazi wenzao wa Jiji la Tanga kutokana na madhara ya kiafya wanayoyapata baada ya kujiingiza kwenye matumizi yake. Ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya kukamata kilo 178 za bangi na kilo 52 za mirungi kwa waandishi wa habari mkoani humo.
Upelelezi wa kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wifred Lwakatare na Ludovick Joseph, umekamilika na jalada lake litapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kwa hatua zaidi.
Jeshi la Polisi mkoani Pwani limefanikiwa kukusanya kiasi cha zaidi ya Shilingi Milioni 825 kutokana na makosa madogo madogo ya barabarani kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mwinyihaji Makame amesema ushiriki wa wananchi katika Ulinzi Shirikishi kupitia Polisi Jamii umeleta mafanikio katika kupunguza vitendo vya uhalifu nchini