| BP YAMWAGA MSAADA KWA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI. |
|
Jeshi la Polisi Tanzania limepokea Msaada wa Kamera 20 na vitabu kutoka Kampuni ya mafuta ya Puma Energy Tanzania LTD (zamani BP) kwa ajili ya kusaidia kazi za Kikosi cha Usalama barabarani nchini wenye jumla ya shilingi Milioni 30.
Msaada huo ulipokelewa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Paul Chagonja kwa niaba ya Inspekta Jenerali wa Polisi ambapo ametoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano wa kampuni hiyo kwa kuwa suala la usalama barabarani ni mtambuka hivyo ni jukumu la kila mtu. Aliwataka Makamanda wa Polisi kuendeleza juhudu za kupata misaada kutoka kwa wadau kwakuwa kwakufanya hivyo haimaanishi kuwa Jeshi la Polisi ni ombaomba bali ni utekelezaji wa maboresho ndani ya Jeshi ambao unamtaka kila mwananchi kushiriki katika ulinzi na usalama (Polisi Jamii/Ulinzi shirikishi) Aidha aliwashukuru wananchi wote kwa kuadhimisha sikukuu ya Krismas kwa amani na utulivu na kuwataka kuendelea hivyo hivyo katika sikukuu ya mwaka mpya wa 2012 ambapo ametoa wito kwa wale walioko mabondeni kufuata ushauri unaotolewa na Serikali wa kuwataka kutorejea katika maeneo ya mabondeni yaliyokumbwa na mafuriko hivi karibuni.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Puma Energy Tanzania LTD aliishauri serikali kulitangaza suala la ajali kama moja ya majanga makubwa yanayotukabili hivi sasa na hivyo basi kuifanya kama ajenda ya kuzungumzwa kwa kina katika ngazi mbalimbali za uongozi
|
