|
1. NIA YETU NI: KUHAKIKISHA USALAMA, HAKI, AMANI NA UTULIVU NCHINI.
2. MALENGO YETU NI: KUFANYA KAZI NA JAMII YETU PAMOJA NA WADAU WENGINE, HIVYO JESHI LA POLISI LITAHAKIKISHA YAFUATAYO:-
-
Kupunguza uhalifu na vitendo visivyokubalika na jamii.
-
Kuhakikisha kuwa wahalifu wote wanakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.
-
Kuwasikiliza wananchi na kujenga imani zao kwa kile tunachokifanya.
-
Kuwasaidia wananchi kuwa salama na kuwafanya wajihisi kuwa wako salama kupitia mkakati wa Ulinzi Shirikishi/ Polisi Jamii (Community Policing Programme).
-
Kufanya kazi kitaalam, kuwajali wananchi na kuwaonyesha uwajibikaji katika kutoa huduma kwa waathirika wa matukio ya uhalifu.
-
Kujenga imani na kujiamini kwa wananchi.
-
WATU WETU (WAFANYAKAZI WA POLISI):
-
Maafisa wakaguzi, askari wa vyeo vyote pamoja na wafanyakazi raia ambao wanaunda Jeshi letu la Polisi ni bidhaa muhimu sana kwetu, ni lazima kuzingatia kuwa na watu sahihi, wenye taaluma sahihi na wamewekwa kwenye maeneo sahihi ili kutoa huduma ya Polisi iliyobora kwa wananchi wote Tanzania.
“The Police officers and civilian staff that make up the Police Force are our greatest asset and it is important that we have the right people with the right skills in the right place to deliver the best possible police service for all Tanzania citizens.”
-
. VIPAUMBELE:Kufanya kazi na jamii yetu na wadau wengine, hivyo Jeshi la Polisi linatekeleza yafuatayo:-
-
Kufanyakazi kwa kuzingatia maadili
-
Kutenda haki kwa kila mtu, kwa kumheshimu na bila kumuonea
-
Kutoa huduma bora (kufanyakazi kwa kiwango)
-
Kuhimiza ushirikiano kama timu bora
-
Kumfanya kila mtu awajibike
-
Kutumia rasilimali zetu kikamilifu.
-
Utayajua maboresho ya Jeshi la Polisi kwa undani zaidi kama ilivyofafanuliwa hapa chini:-
MAENEO YA KUBORESHWA
|
ENEO LINALOLENGWA KUBORESHWA
(KRA)
|
MIKAKATI YA KUFIKIA LENGO
(Broad Intervention)
|
|
1. Mifumo ya kuzuia, kupambana na uhalifu na utendaji wa kazi za polisi (Systems for Improving Policing Operations).
|
-
Kuboresha Mifumo ya Kuzuia uhalifu. (Develop and Institutionalize systems for crime prevention).
-
Kuboresha Mifumo ya Kutanzua uhalifu. (Develop and Institutionalize systems for crime solving)
-
Kuboresha mifumo ya utendaji wa ndani wa jeshi la polisi (Develop and Institutionalize systems for Internal operation).
|
|
2. Sheria, Kanuni na Muundo wa Kitaasisi (Legal, Regulatory and Institutional Structure).
|
-
Kuimarisha uwezo wa taasisi zinazosimamia Jeshi la Polisi (Strengthen the capacity of police oversight and compliance institutions);
-
Kuwezesha Mapitio na Uundwaji wa Sheria na Kanuni (Facilitate review and enactment of laws and regulation);
-
Kujenga na kuboresha muundo wa jeshi (Restructure and re-organize the force).
|
|
ENEO LINALOLENGWA KUBORESHWA
(KRA
|
MIKAKATI YA KUFIKIA LENGO
(Broad Intervention)
|
3. Matumizi Ya Teknolojia Ya Habari Na Mawasiliano (Information and Communication Technology).
|
-
Kuimarisha na kuongeza miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Strengthen and expand ICT infrastructure);
-
Kuimarisha matumizi ya TEKNOHAMA Katika utendaji wa kazi za Polisi (Use of ICT to re – engineer delivery of police services).
|
4. Mifumo ya Menejimenti ya Rasilimali Watu (Human Resource Management).
|
-
Kuhuishwa Kwa Muundo wa Utumishi wa Jeshi la Polisi (Strengthen HR processes and Systems);
-
Kuimarisha usimamizi na utawala wa taarifa za Rasilimali watu (Strengthen the Management of HR information);
-
Kujenga mfumo wa uongozi (Develop TPF Leadership);
-
Kupambana na maambukizi ya UKIMWI ndani ya Jeshi la Polisi (Combat HIV/AIDS in the police force);
-
Usawa wa Kijinsia (Address Gender Inequality in the force).
|
|
ENEO LINALOLENGWA KUBORESHWA
(KRA
|
MIKAKATI YA KUFIKIA LENGO
(Broad Intervention)
|
5. Miundombinu na Vifaa katika Utendaji wa Kazi za Polisi (Infra-structure, Tools and Equipment for Effective Policing).
|
-
Kuakarabati nyumba na miundombinu iliyopo na kujenga mipya (Rehabilitate existing infrastructure and develop new ones);
-
Ununuzi wa vitendea kazi (Acquire new and modern tools and equipment and enhance maintenance capacity).
|
|
6. Ushirikishaji Jamii katika ulinzi na usalama (Involving the Community in Policing).
|
-
Kuwezesha utungwaji wa Sera ya Ushirikishwaji wa Jamii katika ulinzi na usalama (Facilitate the development of a policy framework on involvement of the community in the policing function);
-
Kuimarisha uhamasishaji wa Polisi Jamii (Reinforce community policing awareness campaigns);
-
Kuimarisha uwezo wa Jamii katika kuzuia na kukabiliana na uhalifu (Strengthen the capacity of the community to prevent and solve crime);
-
Kuwajengea uwezo Polisi kufanya kazi na Jamii (Strengthen the capacity of the police to work with the community).
|
|
ENEO LINALOLENGWA KUBORESHWA
(KRA
|
MIKAKATI YA KUFIKIA LENGO
(Broad Intervention)
|
|
7. Usimamizi na Uratibu wa Programu ya Maboresho (Program Governance and Management Arrangements).
|
-
Kusimamia utekelezaji wa Program ya Maboresho (Manage the implementation of the reform program );
-
Kuweka usimamizi wa Programu ya Maboresho (Provide Oversight to the reform program)
-
Kuratibu uhusiano wa programu hii na program zingine za maboresho (Coordinate TPFRP with other reforms);
-
Mfumo wa tathmini na ufuatiliaji wa utekelezaji wa program ya maboresho (Monitor and evaluate implementation of the TPFRP).
|
-
NANI ANAHUSIKA KUBORESHA POLISI
-
Kila Afisa, Mkaguzi, Askari pamoja na watumishi raia kwa jukumu alilopewa, yeye binafsi anawajibika kutekeleza kazi hiyo kwa kuzingatia NIA YETU, MALENGO YETU NA VIPAUMBELE VYETU KATIKA MABORESHO.
-
Kila Kiongozi kwa cheo, wadhifa na majukumu yake anawajibika kusimamia utekelezaji wa MABORESHO kwa mfano. Mkuu wa Polisi Kituo/Kitengo, Mkuu wa Polisi Wilaya, Mkoa hadi makao makuu ya polisi.
HITIMISHO
-
Inawezekana ukiwa na utashi, ubunifu na uthubutu wa dhati ukaleta mabadiliko katika Kitengo/ Kituo, Wilaya/Mkoa na Makao makuu katika eneo la majukumu uliyopewa kutekeleza kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo ya Jeshi la Polisi.
-
Unachotakiwa kufanya ni kufikiri kama mwenye mali na kuthubutu kuwajibika katika majukumu uliyopewa kutekeleza kama unavyojali mali yako binafsi.
-
Tukifikiri kama wenye mali tutaweza kufikia malengo mbalimbali tuliyojiwekea.
|