|
Utii wa sheria Bila Shuruti |
|
RASIMU YA ANDIKO LA MPANGO WA KAMPENI YA UTII WA SHERIA ZA NCHI BILA SHURUTI
UTANGULIZI
Jeshi la Polisi Tanzania kwa kushirikiana na wadau wakewa HAKIJINAI, limeanzisha kampeni ya kuiwezesha jamii kutambua umuhimu wa utii wa sheria za nchi na taratibu za jamii bila shuruti.
Kampeni hii ni moja ya juhudi zinazolenga kuboresha maadili ya jamii kama msingi wa maendeleo yanayozingatia usalama, amani na utulivu ambazo ni nguzo za ustawi wa kijamii, kiuchumi na kiutamaduni.
Msingi wa kampeni hii unalenga kuongeza ari na moyo wa uzalendo unazingatia uwajibikaji katika harakati za kujiletea maendeleo bila kuvuja sheria za nchi.
LENGO KUU
Kuongeza kiwango cha utii wa sheria za nchi bila shuruti jambo ambalo litasaidia kupunguza uhalifu na matumizi ya shuruti katika usimamizi ya utiifu wa sheria za nchi. Utaratibu huu pia utasaidia kupunguza gharama katika oparesheni za kupambana na uhalifu.
Aidha, utii bila shuruti utasaidia kupunguza msongamano wa kesi mahakamani na idadi ya wafungwa/mahabusu wanaotakiwa kuhudumiwa na Idara mbalimbali kwa kodi za wananchi.
|
|